The House of Favourite Newspapers

Gomes Atuliza Mzuka Simba

0

KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes ametuliza mzuka kikosini hapo na kufungukia hali za nyota wake watatu ambao ni nahodha John Bocco, beki wa kati Joash Onyango na Taddeo Lwanga ambao walipata majeruhi katika mazoezi.


Kwa sasa Simba imeweka
kambi nchini Morocco ikiendelea na maandalizi ya msimu mpya wa 2021/22. Wao ni mabingwa watetezi na wanajiadaa na mechi za kimataifa wakiwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Taarifa kutoka nchini Morocco ilieleza kuwa, nyota hao walikuwa wakisumbuliwa na majeraha lakini kwa sasa hali zao zinaendelea vizuri.

 

Gomes alisema: “Ni wachezaji watatu wanasumbuliwa na majeraha ambao ni John Bocco, Taddeo Lwanga na Joash Onyango, majeraha yao sio ya kutisha. Maandalizi kwa ujumla yanakwenda vizuri.

 

Leave A Reply