Gomes Awataja Watakaoimaliza Jwaneng

LICHA ya nyota wake Chris Mugalu kutokuwa fiti kwa asilimia 100 kuwavaa Jwaneng Galaxy ya Botswana kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes amewataja wachezaji anaoamini watafanya kazi ya kuwamaliza wapinzani wake hao.

 

Kesho Ijumaa, kikosi hicho kinatarajiwa kuelekea Botswana kwa ndege binafsi kwa ajili ya mchezo wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 17, mwaka huu.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Gomes alisema: “Ukitazama kuhusu Mugalu bado hajawa fiti kwa kuwa alipata maumivu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji, lakini bado wapo wengine ambao wanaweza kutimiza majukumu yao na ninapenda kazi zao.

 

“Yupo John Bocco, huyu huwa anaweza kucheza vizuri pia akiwa na Meddie Kagere, hapo unaona kwamba bado hata Kibu Denis ambaye sikuweza kumtumia kwenye mechi zilizopita sijamzungumzia, lakini ninaamini kwamba atakuja kuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi chetu.

 

“Sadio Kanoute kiungo huyu ni mzuri hasa akiwa na mpira na anaonekana anapenda kuona matokeo yakipatikana, ninapenda uwepo wake na namna alivyo na jicho la pasi kwa kuwa ameanza kuimarika basi tutajua namna itakavyokuwa mbele ya wapinzani wetu ila sisi tupo tayari.”

Lunyamadzo Mlyuka, Dar es Salaam2176
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment