LondonUpdates: Moto Wa Ghorofa La Grenfell Tower London Waua Watu 12 (Pichaz + Video)
WATU 12 wamethibitishwa kufa katika moto uliolitekeleza jengo la ghorofa 27 la Grenfell Tower jijini London, Uingereza, ambao ulilikumba tangu usiku wa kuamkia jana. Vilevile makundi kadhaa ya watu, wakiwemo watoto na wazee bado hawajulikani walipo katika jengo hilo la eneo la White City ambapo watu zaidi ya 79 walikimbizwa hospitali kwa matibabu.
Ghorofa hilo ambalo lina wakazi 600 lilikumbwa na taharuki kubwa ambapo watu walijaribu kila njia kujiokoa na moto huo ambao ulianza usiku wa manane ambapo ving’ora vya kuashiria moto katika jengo hilo havikufanya kazi, vyombo maalum vya kunyunyiza dawa ya kuzima moto navyo havikufanya kazi na njia maalum ya dharura ya kupita wakati wa majanga ya moto, ilikuwa imezibwa.
Hata hivyo, moto huo hatimaye ulifanikiwa kuzimwa jana na vikosi vya zimamoto na kuliacha jengo likiwa limeungua vibaya.
Wataalam wa masuala ya moto wamesema kwamba wamiliki wa jengo hilo walikuwa walipewa onyo mara kwa mara kuhusu kuta zenye matabaka mbalimbali ambayo yangeweza kusababisha moto mdogo ukawa mkubwa. Hata hivyo, inasemekana wamiliki hao hawauufanyia kazi ushauri huo.
Waokoaji wakiwa wamembeba mtu aliyepata madhara ya moto huo
Baadhi ya waliokumbwa na moto huo baada ya kuokolewa
Walioathirika na moto huo wakilia huku polisi wakifanya doria
Kikosi cha Zima Moto kikiwa kazini
Waathirika wa moto huo baada ya kuokolewa wakiwa na vifurushi walivyofanikiwa kuokoa
Baadhi ya watu waliookolewa
Binti aliyeokolewa akilia kwa uchungu baada ya kuokolewa, hapo anapiga simu kuwasiliana na ndugu zake
Jengo likiteketea kwa moto baada ya kukolea
Baadhi ya maiti zikiondolewa eneo la tukio