Group la Rafiki Connet Walivyojionea maajabu ya Hifadhi ya Pugu Kazimzumbwi
Jumamosi iliyopita Grupu la Watanzania wanaofanya kazi na Kampuni ya Utalii ya Rafiki Connect walitembelea hifadhi hiyo na kujionea mambo mbalimbali ikiwemo pango kubwa la popo ambao kila siku majira ya usiku wote kwa pamoja wanatoka kwenye pango hilo na kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutafuta chakula na kurudi.
Maajabu yaliyopo kwenye msitu huo ni mengi ikiwemo eneo la matabiko ya kizaramo ambapo hutakiwi kufika eneo hilo kama hauko safi yaani usiwe umevuta bangi wala kuchepuka bila kuoga.
Sifa ya kumaliza kutalii hifadhi hiyo ni kupandisha mlima huo mpaka kileleni na kuliona vizuuuri jiji la Dar es Salaam lakini kasheshe kubwa ni jinsi ya kufika kileleni hapo. HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL