The House of Favourite Newspapers

GSM Aridhia kushiriki kufanikisha ujenzi wa uwanja wa kisasa wa Yanga

0

RAIS wa klabu ya Yanga Injinia Hersi SAID amethibitisha kuwa mdhamini na mfadhili wa Klabu ya Yanga, Ghalib Said Mohammed (GSM) ameridhia kushiriki kufanikisha ujenzi wa uwanja wa kisasa wa Young Africans Sports Club, katika eneo la Makao Makuu ya Klabu yetu, Jangwani, Jijini Dar Es Salaam.

Injinia Hersi ameyasema hayo leo Februari 11, 2024 Mkoani Mbeya kwenye sherehe za miaka 89 za kuzaliwa kwa Klabu hiyo kongwe na yenye mafaniko zaidi nchini Tanzania.

“Baada ya mazungumzo ya muda mrefu na mdhamini na mfadhili wa Klabu yetu, Ghalib Said Mohammed (GSM), nipende kuwataarifu Wanachama na Mashabiki wa Klabu yetu kuwa leo, GSM ameridhia kwa dhati kushiriki kwenye kufanikisha ujenzi wa uwanja wa kisasa wa Young Africans Sports Club, katika eneo la Makao Makuu ya Klabu yetu, Jangwani, Jijini Dar Es Salaam.” Injinia Hersi

“Nichukue fursa hii kumshukuru sana GSM kwa dhamira hiyo inayokwenda kutimiza ndoto ya Uongozi wangu, Kamati ya Utendaji na Wanachama na Mashabiki wa Young Africans kwa kuwa na uwanja wetu.”

“Kwa niaba ya Uongozi, Wanachama na Mashabiki wa Young Africans SC, nipende kumuahidi GSM, kuwa tutampa ushirikiano wote utakaohitajika kuhakikisha tunafanikisha ujenzi wa uwanja wetu.”

Leave A Reply