The House of Favourite Newspapers

Makonda Asimamisha Ziara Na Kuungana Na Watanzania Katika Siku 5 Za Maombolezo Kufuatia Kifo Cha Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa

0

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda amesimamisha ziara yake ya Mikoa 20 Back To Back na kuungana na Mwenyekiti wa CCM na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Watanzania wote kwa ujumla katika siku 5 za Maombolezo ya Aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Edward Ngoyai Lowassa.

Makonda ametoa wito kwa Watanzania wote kwa ujumla kuungana na Familia na Ndugu wa Marehemu katika kuwaombea wanapopitia kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Aidha, Makonda ametoa rai kwa Viongozi wengine wa vyama mbalimbali vya siasa kuachana na shughuli zingine zote za kisiasa na kuungana katika maombolezo ya msiba huu mzito wa Taifa.

Ratiba ya muendelezo wa ziara itatolewa baada ya kumalizika kwa Maombolezo haya.

Leave A Reply