GSM Yafanya Kufuru Yanga, Mastaa Wanunuliwa Magari

ACHANA bonasi wanazoendelea kuzitoa wadhamini wa Yanga, Kampuni ya GSM, kubwa kuliko ni wachezaji wa timu hiyo kununuliwa magari ya kisasa ya kutembelea.

 

Hivi karibuni, GSM ilimaliza kabisa sakata la utoaji bonasi kwa mastaa wa timu hiyo kutokana na ahadi walizoweka ikiwemo ile ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba.

 

Mmoja wa mabosi wa Yanga, ameliambia Spoti Xtra kuwa, karibia wachezaji wote wa timu hiyo hivi sasa wanamiliki magari binafsi wanayotumia katika mizunguko yao.

Bosi huyo alisema kuwa, baadhi ya wachezaji magari yao wamenunuliwa na mdhamini wa timu hiyo, Bilionea, Gharib Salim Mohammed (GSM), huku wengine wakinunua kutoka katika bonasi wanazopata.

 

Alisema kuwa, wachezaji saba wapya wa kigeni ndiyo bado hawajanunuliwa, lakini hadi kufikia Desemba, mwaka huu watakuwa wanamiliki ya kwao baada ya kukamilisha ishu za leseni ambao ni Djigui Diarra, Shaban Djuma, Fiston Mayele, Jesus Moloko, Khalid Aucho, Yannick Bangala, Heritier Makambo na mzawa Yusuph Athumani.

 

Aliwataja wachezaji wa mwisho kununuliwa magari ni Kibwana Shomari, Dickson Job, Feisal Salum ‘Fei Toto’ na Ramadhani Kabwili ambao wote hivi sasa wanamiliki magari aina ya Toyota Athlete Crown.

 

Wengine wanaomiliki Crown ni Mukoko Tonombe na Farid Mussa.Said Ntibazonkiza ‘Saido’ anamiliki Toyota Mark X, Deus Kaseke (Toyota Ractis), huku waliobaki wakiwa na Toyota IST akiwemo Ditram Nchimbi.

 

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, alipotafutwa na Spoti Xtra kuzungumzia hilo, alisema: “Hayo ni maisha binafsi ya wachezaji wetu kumiliki magari, hivyo ni ngumu kuzungumzia hilo kwa kina. Bonasi za wachezaji wetu ni siri kati ya uongozi na wachezaji.

MACHINGA NA MBINU MPYA KIBIASHARA, | CCTV YAIBUA MAZITO KESI YA SABAYA | FRONT PAGE.2176
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment