The House of Favourite Newspapers

Guardiola Awahofia Mastaa Man U, Kucheza Etihad Leo

0

BOSI wa Manchester City, Pep Guardiola amekiri kuwa wapinzani wao Manchester United ni tishio kwani wamekamilika kila kila idara huku akimhofia Bruno Fernandes.

 

Man City, leo Jumapili itaikaribisha Man United kwenye mchezo wa Premier League ambao utapigwa katika Uwanja wa Etihad.

 

Guardiola amesema pamoja na kuwa timu yake inaonekana kuwa katika ubora, bado wapinzani wao ni tishio kwani wanaweza kufanya lolote kwani wapo imara kila idara.

 

Timu hizo zinaenda kukutana wakati Man City imecheza mechi 28 bila kufunga na ikishinda mechi 21 mfululizo na Man United wakiwa na rekodi ya kutopoteza mechi 21 ugenini.Guradiola alisema:

 

“Man United wapo imara kila idara ya ulinzi wapo vizuri, katika eneo la ushambuliaji Bruno Fernandes ana spidi kama ilivyo kwa (Dan) James, (Marcus) Rashford na (Anthony) Martial.

 

“Pia uzoefu wa Cavani pia utawabeba United na huyu ni mchezaji ambaye nina mkubali kutokana na rekodi zake kwenye soka.

 

“Kwa maana hiyo bado United tunaenda kucheza nao wakiwa ni tishio kwa upande wetu hivyo tunatakiwa kuwa makini.” Kwa upande wa Ole Gunnar Solskajer wa Man United, alisema: “Tunaenda kupambana na timu bora, lakini malengo yetu yanabaki kuwa ni kushinda kila mchezo uliopo mbele yetu.”

Leave A Reply