The House of Favourite Newspapers

Guinness Smooth yatanua soko lake Kanda ya Ziwa

0

Mwanza, Machi 29, 2022:

Bia ya Guinness Smooth, mwanafamilia mpya wa Guinness nchini Tanzania, inaongeza soko lake kwa kasi sana nchini na safari hii ni zamu ya Kanda ya Ziwa, shukrani kwa Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa ubunifu huo mpya.

 

Bia ya Guinness Smooth inaingia Kanda ya Ziwa ikiwa ni  baada ya uzinduzi wa bia hii katika mikoa ya Kaskazini na Kusini mwa Tanzania.

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kinywaji hiki, uzinduzi uliyowakutanisha wasambazaji na wamiliki wakuu wa migahawa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, Meneja Bidhaa wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Ester Raphael alisema, familia ya Guinness, Tanzania inajivunia kutambulisha bia mpya ya Guinness Smooth katika Kanda ya Ziwa, kanda ambayo ni ngome za bidhaa za SBL hapa nchini.

 

Guinness Smooth ni bia mpya katika familia maarufu ya Guinness. Bia hii ina ladha laini ya kuburudisha, nyororo na yenye uwiano kamili wa ladha ambazo ni bora kwa kufurahia huku ukiwa na marafiki, wakati wowote na mahali popote. Kinywaji hiki kina viburudisho vyote vilivyo ndani ya kinywaji maarufu cha Guinness.

 

“Kutoka  Dar es Salaam, Kaskazini,  kati hadi Kusini na sasa Kanda ya Ziwa, Guinness Smooth sasa inabisha hodi Mwanza na Kanda nzima ya Ziwa ikiwa na mengi ya kutoa kwa wakazi wa kanda hii. Kiywaji hiki kinaleta uzoefu mpya kupitia ladha yake bora,” alisema Bi. Ester Raphael.

 

Katika hafla ya uzinduzi wa kinywaji hiki, kivutio kikubwa kilikuwa bia hii yenyewe kufuatia muonekano na ladha yake sawia.

 

Ikiwa imetengenezwa kwa kuangalia mandhari ya soko la Tanzania, Bi. Ester Raphael anasema, Guinness Smooth ni usemi mpya ndani ya Guinness uliotengenezwa na watengenezaji bia wakuu wa Guinness wa ndani na nje ya nchi, ili kutoa bia ya kusisimua na ya kipekee ambayo ni kamili kwa hafla za kawaida za kijamii.

 

“Bia hii laini inazalishwa hapa Tanzania katika kiwanda chetu cha bia Moshi,” Alifafanua

 

Guinness ina utamaduni na uzoefu wa muda mrefu wa kutengeneza bia maridhawa, bia zenye ladha ya kuvutia na kuridhisha tangu mwaka 1759.

“Guinness Smooth mpya inaendelea kuthibitisha dhamira ya SBL ya kuwaletea watumiaji bia zenye ladha nzuri wanazoweza kufurahia katika mikusanyiko yote ya kijamii,” alisema Ester Raphael na kuongeza: “Kinywaji hiki ni bia maalum inayoburudisha ambayo unatakiwa kuifurahia unapokutana na marafiki. Nakutakeni mburudishwe na bia yetu hii ya Guinness Smooth.”

 

 

MWISHO//

 

Kuhusu Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL):

Kampuni hii ilianzishwa mwaka 1988 kama Kampuni Shiriki ya Bia, na sasa ni ya pili kwa ukubwa nchini Tanzania. Kampuni hii inayo matawi ya uzalishaji matatu yaliyo jijini Dar es Salaam, Mwanza na Moshi.

Tangu kuanzishwa kwa Kampuni ya Bia Serengeti 2002, kampuni hii imekuwa huku ikianzisha bidhaa mbalimbali mwaka hadi mwaka. Upatikanaji wa Hisa kutoka EABL/Diageo mwaka 2010 umeongeza uwekezaji katika viwango vya ubora wa Kimataifa ndani ya kampuni hii na kuongeza idadi ya ajira kwa Watanzania.

Bidhaa za SBL zimekuwa zikipokea tuzo mbalimbali za kimataifa zikijumuishaSerengeti Premium Lager, Serengeti Lite, Pilsner Lager, Pilsner King, Tusker Lager, Tusker Lite, Kibo Gold, Guinness stout na Kick. Kampuni hii pia ni nyumbani kwa vinywaji vikali duniani kama vile Johnnie Walker Whisky, Smirnoff Vodka, Gordon’s Gin, Captain Morgan Rum na Baileys Irish Cream.

 

Kwa Taarifa zaidi wasiliana na;

 

John Wanyancha

SBL Mkurugenzi wa Mawasiliano

Simu: 0692148857

Barua pepe: [email protected]

 

Leave A Reply