The House of Favourite Newspapers

Guinness Smooth Yazinduliwa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na ‘Vibe’ la Kutosha

0
Meneja uvumbuzi wa Kampuni ya bia ya Serengeti Bertha Vedastus akigonganisha glasi na wateja wa kampuni hiyo waliofika katika uzinduzi wa bia ya Guinness Smooth uliofanyika jijini Mbeya.

 

 

WAKAZI wa Mbeya na eneo zima la kanda ya Nyanda za juu kusini, sasa wanaweza kufurahia ladha ya kipekee ya bia ya Guinness smooth kutoka katika baa iliyo karibu nao baada ya uzinduzi rasmi wa bia hiyo.

Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, wakisakata sebene muda mfupi baada ya uzinduzi wa bia ya Guinness Smooth uliofanyika jijini Mbeya.

 

 

Guinness smooth ni bia mpya ndani ya familia  kubwa na kongwe duniani ya Guinness. Bia hii inaladha murua ambayo huwafanya watumiaji wake kuifurahia kila mara wanapoitumia ikiwa na sifa zilizoongezwa vionjo za bia ya Guinness.

Burudani zikiendelea eneo la tukio.

 

 

Akiongea wakati wa uzinduzi wa bia hiyo uliofanyika jijini Mbeya, meneja uvumbuzi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti ambao ndiyo watengenezaji wa bia hiyo alisema uzinduzi huo wa kanda za nyanda za juu kusini unafanyika baada ya uzinduzi uliokuwa na mafanikio wa Dar es Salaam na kanda ya kaskazini.

Meneja uvumbuzi wa Kampuni ya bia ya Serengeti Bertha Vedastus akiongea na wateja wa kampuni hiyo wakati wa uzinduzi wa bia ya Guinness Smooth uliofanyika jijini Mbeya.

 

 

“Wakazi wa kanda ya Nyanda za juu kusini wamekuwa ni waaminifu kwa bidhaa za SBL na kwa namna ya pekee tuwashukuru kwa kuchagua bidhaa zetu.

 

 

Ikiwa kama sehemu ya kuwaonyesha mapenzi yetu kwao, leo tunawaletea bia mpya ya kimataifa ambayo itawapa uzoefu wa kipekee kila wanapoitumia,” alisema.

 

 

Meneja uvumbuzi huyo alisema alisema bia ya Guinness Smooth imetengenezwa kwa kumjali mtumiaji bia wa Kitanzania ikiwa na ladha ya kipekee na kuongeza kuwa bia hiyo inatengenezwa kwa kiasi kikubwa cha malighafi za ndani kwenye kiwanda cha SBL kilichopo Moshi mkoani Kilimanjaro.

 

 

Bertha alisema bia mpya ya Guinness Smooth inathibitisha nia ya kampuni ya bia ya Serengeti kuwapatia bidhaa bora zenye viwango vya kimataifa lakini katika bei ambayo kila mtu aweze kuimudu.

Leave A Reply