Gumzo Manara Kuondoka Simba “Asanteni, Imetosha”

SINTOFAHAMU imetanda baada ya kuwepo kwa tetesi kuwa msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara kudaiwa kujiuzulu. Hayo yamejili baada ya Manara kuposti kwenye ukurasa wake wa Instagram maneno haya ambayo yametafsiriwa na wengi kuwa amebwaga manyanga.

 

“Hivi vitimbi mnavyonifanyia kila siku kisa Simba vishanichosha, mwisho wa siku mtanitoa roho yangu kabla ya muda wangu…
Imetosha kwa sasa!! Ubaya wote ni Haji lakini mafanikio ni yenu nyie Wakubwa… Kila siku ni Haji Haji Haji…

 

“Mkitoka kunisingizia hili mtatengeneza cinema nyingine kwangu,,tunashindwa kujua kila Mja Mungu kampa fungu lake,,,,inakuwaje Rizki ya umaarufu wa mwenzio iwahangaishe kiasi hcho?

 

“Likinitokea baya pakuanzia mnapo. Asanteni ndugu zangu na Mlipaji ni Mungu na ukweli utajulikana. IMETOSHA,” amendika na kuibua gumzo mtandaoni juu ya kile kilichomsibu.

@manyota_rich3403
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment