The House of Favourite Newspapers

GWAJIMA AMWAMBIA JPM: NILIPEWA BAKULI LA ALMASI – VIDEO

MCHUNGAJI wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima amemshauri Rais Dkt. John Magufuli kuunda timu ya watu wenye uzoefu mkubwa na wanaoijua siasa ya madini kimataifa, ili kuweza kupata soko kubwa zaidi.

 

Mch. Gwajima ametoa ushauri huo alipokuwa akizungumza mbele ya Rais Magufuli kwenye mkutano mkuu wa kisekta wa wizara ya madini na kwamba ni vyema akaunda timu ya watu wenye ‘exposure’ kwenye siasa ya madini, kwani itasaidia kuweza kupenya kwenye soko la kimataifa.

 

“Leo umekuwa kama Nabii, nitoe ushauri kwa Mh. Rais, si kweli kama hakuna soko la madini, dhahabu yenyewe ni fedha, isipokuwa nashauri kama ikikupendeza, uwe na watu wenye exposure kwenye siasa za madini kimataifa, sisi kwa asili tuna dhahabu, huwezi kutuambia tumechukua dhahabu ya wengine tuthibitishe ni za kwetu, hizo ni siasa tu za masoko, unaweza ukaunda watu wenye exposure ambao wanaweza kufikia masoko mbali mbali duniani”, amesema Askofu Gwajima.

 

Sambamba na hilo Mchungaji Gwajima ameendelea kueleza kwamba madini tuliyonayo ni mengi na yanakosa soko kutokana na sababu mbali mbali, na iwapo yangelipiwa ushuru yasingezagaa, hivyo kama ambavyo aliwahi kukutana nayo watu wakiyauza kwenye bakuli barabarani.

 

“Nilipita Mwadui nikashangaa, wakaniuliza tukuletee almasi kwa utani, ndani ya saa moja watu walileta almasi imejaa bakuli haina watu wa kununua, wametoka nazo ndani ya nyumba zao, hizo kama zingelipiwa ushuru nchi yetu ingekuwa mahali pazuri sana”, amesema Gwajima.

 

Leo Jumanne, Januari 22, 2018, Rais Magufuli amefanya Mkutano na wadau wa Sekta ya Madini, ambao pia uliwakutanisha na wadau na wafanyabiashara ya madini yaliyopo nchini.

Comments are closed.