The House of Favourite Newspapers
gunners X

Gwajima Atinga Bungeni Chini ya Ulinzi Mkali – Video

0

MBUNGE wa Kawe, Askofu  Josephat Gwajima leo Agosti 23 ametii wito kufika mbele Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Kinga na Mamlaka ya Bunge ili kujibu tuhuma mbalimbali ikiwemo kusema uongo na kushusha hadhi na heshima ya bunge.

 

Gwajima ambaye ni Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, amewasili Viwanja vya Bunge Majira ya saa 6:40 mchana huu kuitikia wito wa kamati hiyo kufuatia wito wa Spika wa Bunge, Job Ndugai aliyemtaka mbunge huyo pamoja na Mbunge mwenzake, Jerry Slaa wa Ukonga kufika mbele ya kamati.

 

Gwajima amekuwa na msimamo wa kupinga chanjo ya corona na kusema waziwazi kuwa yeye na familia yake hawatochanjwa chanjo hiyo hata kama Bunge likilazimisha, hatochanjwa.

 

Akizungumza katika ibada zake kadhaa za  Jumapili, hivi karibuni, alisema chanjo hiyo inayoendelea kutolewa nchini hazijafanyiwa utafiti wa kina kubaini madhara yake kwa wanaochanjwa na vizazi vijavyo na kwamba chanjo hiyo bado ipo kwenye majaribio.

 

Leave A Reply