The House of Favourite Newspapers

H Baba Amtetea Harmonize, Amuumbua Mwijaku Kisa Binti Yake Paula Kajala

0
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva,H Baba.

H Baba; ni msanii wa muziki wa Bongo Fleva ambaye hivi karibuni alionekana kuwa kinyume na aliyekuwa bosi wake kwenye Lebo ya Konde Gang, Harmonize, lakini safari hii amemtetea huku akimuumbua mtangazaji Mwijaku.

 

H Baba anamtetea Harmonize dhidi ya matamshi ya Mwijaku kwamba aliingia katika sebule yake na kumkuta binti Paula Kajala akimkanda kifuani.

 

H Baba anamsuta Mwijaku kwa tabia ya kuingia kwenye sebule za watu na kuanza kutoa mambo ya ndani mwa watu na kuyaweka wazi kwa umma.

Bosi wa Lebo ya Konde Gang, Harmonize akiwa na mpenzi wake Kajala.

Anasema kuwa, katika hilo anamtetea Harmonize kwa vile mambo ambayo wanafaa kuchafuana ni ya nje tu na wala si ya ndani ambayo yanapaswa kubaki kuwa siri za watu husika wenyewe.

 

H Baba anakanusha madai kwamba huenda Mwijaku ametumwa na Diamond ili kumchafulia jina Harmonize na kusema kwamba kama ana namba ya Diamond, basi hajawahi kuzungumza na yeye moja kwa moja.

 

“Diamond hana muda mchafu na mimi nasema leo, kama ana namba ya Diamond, anayo sawa, lakini Diamond hapokei simu ya Mwijaku na hajawahi kupokea simu yake. Mwijaku anaonana na watu wa chini tu wala hawezi kuonana na Simba. Wanakutana tu kwenye shoo,” anasema H Baba.

Stori; Khadija Bakari, Dar

UKWELI HARMONIZE KULA KUKU NA MAYAI, ZUCHU MJAMZITO | HOTPOT

Leave A Reply