The House of Favourite Newspapers

Haaland Mchezaji Pekee Aliyefuta Kiburi Cha Guardiola

0

Mshambuliaji Earling Haaland ndio mchezaji pekee ambaye amefanikiwa kuondoa kiburi cha kocha mtata Pep Guardiola ndani ya kikosi cha Manchester City na hii inatokana na ubora wa mshambulaiji huyo.

Kocha Guardiola licha ya ubora wake lakini anafahamika kama kocha mwenye misimamo yake na asiyekubali kushindwa kwenye jambo lake, Lakini Haaland amefanikiwa kumbadilisha raia huyo wa kimataofa wa Hispania.

Pia kumbuka kuna kucheza JACKPOT ya Meridianbet ambayo inakufanya ushinde shilingi Milioni Mia Mbili, 200,000,000 kwa dau lako la shilingi 1000 pekee ukibashiri kwa usahihi mechi zako 13. Nafasi ni yako ingia www.meridianbet.co.tz na uweke mkeka wako. utakua ni mchezo wa pili kukutanisha vilabu hivyo msimu huu baada ya kukutana

Guardiola anafahamika kama ni muumini mzuri wa mpira wa pasi nyingi maarufu kama Tik Tak ambapo kupitia aina hii ya mpira timu nzima inapaswa kushiriki mchezo, Huku ikiwa haina mchezaji ambaye anasubiria mpira na hashiriki mchezo muda mwingi.

Haaland amekuja kuharibu utaratibu huo kwani mchezaji huyo sio mchezaji ambaye ana uwezo wa kushiriki mchezo kwa kiwango kikubwa kama aina ya mpira wa kocha huyo inavyotaka, Lakini mshambuliaji huyo amefanikiwa kuingia kwenye kikosi cha kocha huyo.

Wakati kocha huyo anafika ndani ya klabu ya Manchester City mshambuliaji Sergio Aguero ndio alikua mshambuliaji namba moja na anayefanya vizuri klabuni hapo, Lakini Guardiola alimuondoa kwakua hakua mshambuliaji ambaye anaendana na aina ya mpira ambao timu yake anataka icheze lakini mambo yamekua tofauti kwa Haaland.

Kutokana na hali hiyo inaonesha kocha Guardiola amekubali kunyoosha mikono kwa Erling Haaland, Kwani sio mchezaji ambaye anafaa kwenye mfumo wake lakini imembidi amtumie na hii ni kutokana na umahiri wa kupachika mabao wa raia huyo wa kimataifa wa Norway.

Pia kumbuka kuna kucheza JACKPOT ya Meridianbet ambayo inakufanya ushinde shilingi Milioni Mia Mbili, 200,000,000 kwa dau lako la shilingi 1000 pekee

ukibashiri kwa usahihi mechi zako 13. Nafasi ni yako ingia na uweke mkeka wako.

Leave A Reply