The House of Favourite Newspapers

Halima Mdee Agoma Kumpa Mkono Dkt. Mashinji – Video

0

ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Dkt Vincent Mashinji, amefika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumatatu, Februari 24, 2020, na kukutana na viongozi wa Chadema kwa ajili ya kusikiliza kesi inayowakabili.

 

Mashinji aliyehamia CCM na viongozi wengine wanane wa chama hicho wanakabiliwa na kesi ya jinai yenye mashtaka 13 yakiwemo ya uchochezi.

Baada ya kuingia mahakamani alianza kuwasalimia waliokuwa viongozi wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti wao Freeman Mbowe, Peter Msigwa, Esther Bulaya na wengine waliokuwepo mahakamani hapo.

 

 

Mambo yalikuwa tofauti kwa Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), Halima Mdee,  ambaye alikataa kumpa mkono wala kumsalimia  Mashinji huku akijifanya yuko bize na simu yake.

Hali hiyo imechukuliwa na baadhi ya watu waliokuwepo mahakamani na kuwa huenda Mdee amechukizwa  na kitendo cha Mashinji kutimkia CCM.

 

Miongoni mwa mashitaka yanayowakabili viongozi hao ni pamoja na  kufanya mikusanyiko na maandamano yasiyo halali.

HALIMA MDEE AMNYIMA MKONO DK. MASHINJI, MAHAKAMANI

Leave A Reply