The House of Favourite Newspapers

HALOTEL KUWEZESHA VICOBA KUWASILIANA BURE

0
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni ya  Halotel, Mhina Semwend (kulia) akizungumza na Waandishi wa habari.
Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.
Baadhi ya wanavikundi vya ujasiriamali waliohudhuria hafla hiyo wakielekezwa namna ya kujiunga na  huduma hiyo mpya ya ‘VICOBA PACK’ kuwasiliana bure ndani ya vikundi vyao.
Baadhi ya wanavikundi vya ujasiriamali waliohudhuria hafla hiyo.

 

 

 

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

 

DAR ES SALAAM;  Kuendelea kukua kwa teknolojia ya Mawasiliano, kumekuwa chachu ya maendeleo katika mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa na kijamii, jambo ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo miongoni mwa Watanzania. Licha ya maendeleo hayo katika sekta hiyo bado makundi mbalimbali ya kijamii hayakuonekana kupewa kipaumbele jambo ambalo bado lilietendela kuleta changamoto katika kuinua tumekuwa tukianzisha huduma ambazo zinalenga makundi husika lengo letu limekuwa ni kwanza kabisa kuonesha utofauti katika utoaji wa huduma za Mawasiliano, pamoja na kuweka urahisi katika huduma hizo kwa Watanzania.

 

“Tunatambua nchi yetu ina vikundi mbalimbali ambavyo vina jishughulisha na Masuala ya kiuchumi, na kijamii, katika yote haya Mawasiliano ni kitu muhimu sana miongoni mwa waanavikundi, kwa umuhimu huo huo, tutawawezesha wanachama wote walio katika makundi husika kuweza kuwasiliana bila ya kuwa na mipaka, lakini Zaidi ya hapo kuchochea maendeleo ya kiuchumi,” Alisema Mkuu huyo wa Mawasiliano na kuongeza.

 

“Ili Watanzania waweze kujiunga na Huduma hii ni lazima wanunue Laini za simu pya za Halotel zitakazosajiliwa kwa jina la kikundi huku wanachama wote watapaswa kuwa na Laini mpya za Halotel ambazo ni maalum kwa ajili ya ofa hiyo, ambayo itawawezesha wanakikundi wote kuwasiliana bure na endapo atahitaji kuwasiliana nje ya Mtandao atatozwa hadi Shilingi 2500/= au 4999/= tu kwa mwezi kulingana na matumizi yake.

 

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Jumuia ya Federation Tanzania Bi. Hadija amesema kuwa wamepokea huduma hiyo kwanza kwa upekee Mkubwa kwani tangu huduma za mawasiliano zimekuwepo, Vikundi vya wajasiriamali havikuwahi kupewa kipaumbele katika Mawasiliano hivyo kuanzishwa kwa huduma hii kutatuwezesha mamilioni ya Watanzania tulio katika vikundi mbalimbali vya wajasiriamali kuweza kuwasiliana kwa urahisi Zaidi, kwa muda mrefu tumekuwa tukisubili huduma za aina hii.

 

Kwa upande wao baadhi wawakilishi kutoka vikundi mbalimbali vya kijamii waliohudhuria Mkutano huo wamefurahishwa na kuzinduliwa kwa huduma hiyo itakayowawezesha kuwasiliana na  wanachama wenzao walio katika vikundi vyao.

 

Ili kujiunga na Huduma hiyo, Wanachama waliokatika vikundi mbalimbali vya kijamii watapaswa kutembelea ofisi za Kampuni hiyo ya simu na kujiunga kwa pamoja ili waweze kuwasiliana, Kampuni hiyo imeahidi kuendelea kusimamia katika kutekeleza kauli mbiu ya kuwa kampuni ya Kwanza inayoongoza kwa kutoa huduma bora na nafuu.

 

 

Leave A Reply