The House of Favourite Newspapers

Hamadai: Zao la THT lililohusika kumtoa Ruby

0

085A0705

Msanii wa THT, Hamad Hassani ‘Hamadai’ akifanya mahojiano na Global Tv Online siku ya jana.085A0708 085A0715 085A0717

Akiwa katika pozi.

085A0720

Mwandishi wa Burudani, Andrew Carlos (kulia) akiwa na Hamadai.

085A0725

Shaban wa Globa TV akiwa na Hamadai.

085A0722

Hilal wa Global TV akiwa na Hamadai.

UNAPOFIKA katika Jumba la Kuinua Vipaji (THT) ukaulizia wasanii wakali wanaotikisa kwa kipindi hiki ni wazi utamtaja Alice na msanii Hamad Hassani ‘Hamadai’.

Hamadai ndiye aliyehusika katika kutengeneza matangazo kibao ya redio likiwemo moja la kituo cha Clouds FM linalojulikana kama Tunakufungulia Njia Kuwa Unachotaka.

JAna Hamadai alitimba ndani ya Global TV Online na kuhojiwa moja kwa moja kupitia kipindi cha Exclusive ambapo alifunguka mambo mengi yahusiyo muziki wake na safari yake hadi kuingia THT.

“Mwanzoni niliona kama kuingia THT ni rahisi lakini nilipofika nilijikuta nikichujwa na wenzangu hadi kufikia hapa nilipo nimekwiva kweli na naweza kusimama mimi kama mini.

“Awali nilianza kusikika kwenye tangazo la Tunakufungulia Njia baada ya kuitwa na uongozi na kuniomba nitunge na kuimba tangazo hilo ambalo linapigwa mara kwa mara kwa sasa kwenye kituo cha Cloud FM,” anasema Hamadai.

Mbali na kujulikana kwenye matangazo, HAmadai anasema kuwa wasanii wengi amekuwa akisaidiana ambao ni Barnaba, Linah na wengine wengi.

“Mfano Wimbo wa Na Yule wa Ruby naweza kusema nimehusika kwa asilimia kubwa katika kurekebisha baadhi ya vitu na hadi unausikia pale,” alimaliza HAmadai anayebamba na Wimbo wa Marioo. Tembelea Global TV Online kutazama mahojiano yake siku ya Jumatatu.

Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL

Leave A Reply