The House of Favourite Newspapers

Bella aungana na TID, Nature kutambulisha Goma la Kimakonde

0

085A0789

Hilal wa Global TV akiwa na Msanii wa filamu na muziki Bongo, Isabela Mpanda.

085A0790

Mwandishi wa Burudani, Andrew Carlos (kushoto) akiwa na Isabela.

085A0796

Walusanga Ndaki akijiachia katika pozi na Isabela.

 MSANII wa filamu na muziki Bongo, Isabela Mpanda ‘Bella Fasta’ ametambulisha wimbo wao wa Goma la Kimakonde kupitia Global Tv Online jana.

Wimbo huo wameimba wasanii wote kutoka kusini wanaojiita Kusini All Stars vikiwemo vichwa kama vile Jay Mo,TID, Juma Nature, Pasha,  Isabela Mpanda, Baby Madaha, Jaffarai, Dullayo, Z-Anto na wengine kibao.

Akizungumza katika kipindi cha Exclusive kupitia Global TV Online, Bella alisema kuwa wimbo huo umewafanya kuwa wasanii wa kwanza wenye muunganiko wa wasanii wengi.

“Ujue Kusini All Stars tupo wengi yaani hapa tukianza kumuongelea mmoja mmoja ni wengi sana kuna wengine walikosa kurekodi lakini tutakuwa nao kwenye wimbo mwingine, mtu kama Jux naye ni mmojawapo,” alisema Bella.

Muunganiko huo unatarajiwa kutoa video ya Wimbo wa Goma la Kimakonde hivi karibuni.

Imeandaliwa na Andrew CArlos/GPL

PICHA NA GLOBAL TV ONLINE

Leave A Reply