The House of Favourite Newspapers

Hans Poppe Atoa Siri Manji Alivyowapoza

0

Wilbert Molandi | CHAMPUIONI|Dar es Salaam

MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe ametamka kuwa kuondoka kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kutawapa nafuu wao.

Kauli hiyo ameitoa ikiwa ni siku chache tangu Manji atangaze kuon­doka kuiongoza Yanga kwa kile ali­chodai kuwapisha wengine kuiongo­za timu hiyo inayojiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Manji tangu ameingia kuiongoza Yanga akiwa kama mwenyekiti wa timu hiyo mwaka 2012, ameipa ma­fanikio makubwa ikiwemo kutwaa mataji matatu mfululizo ya ligi kuu, lakini pia Kombe la FA na Kombe la Kagame mara moja.

Akizungumza na Cham­pioni Ijumaa, Hans Poppe alisema kuwa Manji ndiye alikuwa kikwazo kwao kwenye mambo mbalimbali ikiwemo usajili wa wachezaji kutokana na udhamini mkubwa al­iokuwa anautoa kwenye klabu hiyo.

Hans Poppe amesema mwenyekiti huyo alikuwa anafanikisha kambi za nje ya nchi ikiwemo nchi­ni Uturuki ambayo Simba ilikuwa ngumu kutokana na kukosa udhamini mzuri kama waliokuwa wanaupata Yanga.

“Kama unakumbuka wakati anaingia ma­darakani ni yeye aliye­fanikisha kumtoa Kaseja (Juma) Simba tukiwa tu­namhitaji kwa kumsajili kwa dau la shilingi mil­ioni 50.

“Kingine ni uwezo wake wa kifedha wa kwenda kuiweka timu kambi nje ya nchi ikiwemo Utu­ruki wakati sisi tukiwa hapa nchini, hivyo Yanga watamkumbuka sana.

“Na Yanga watamkum­buka kwa kushindwa kutumia fedha zake za udhamini vizuri, ninaamini kama Yanga wangezitumia vema fedha zake, basi naamini wasingekuwa tegem­eo na wangejiendesha wenyewe,” alisema Hans Poppe na kuongeza:

“Wao walizoea kula ka­tika hoteli za kitalii lakini sasa hivi hawawezi kupa­ta mambo kama hayo, si unaona hata walipokuwa Mwanza katika mch­ezo wao wa mwisho wa Ligi Kuu, uliona hoteli waliyofikia, picha wali­zopiga wakisherehekea ubingwa zilionyesha siyo hoteli kama ambavyo walizoea kufikia wakati wa Manji.

Wakati wa utawala wa Manji, alifanikiwa ku­wasajili Kelvin Yondani kutoka Simba, Mbuyu Twite aliyekuwa akiwan­iwa na Simba na tayari alikuwa amekamilisha baadhi ya makubaliano na Simba.
GLOBAL TV Online, Kupitia kipindi chake cha Michezo, SPOTI HAUSI, kinazungumza EXCLUSIVELY na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Timu ya Soka ya Simba Sport Club, Zacharia Hans Poppe ambaye anafunguka mengi kuangazia klabu yake na soka la bongo kwa ujumla.

FUATILIA MAHOJIANO HAYO HAPA

Leave A Reply