The House of Favourite Newspapers

Harmonize Afunguka Kumsaliti Kajala, Ataja Video ya Wimbo Wake wa ‘The Way You Are’

0
Supastaa wamuziki  wa Kizazi Kipya nchini Tanzania akiwa na mpenzi wake Kajala.

 

Harmonize au Konde Boy; ni supastaa wamuziki  wa Kizazi Kipya nchini Tanzania ambaye nyimbo zake hazikauki midomoni mwa mashabiki wake kwa sasa kutoka na wingi wake.

 

Sasa; habari mpya ni juu ya tetesi za Harmonize au Harmo kumsaliti mchumba wake, Kajala Masanja baada ya kuvuja kwa video ya jamaa huyo akiwa na aliyekuwa mpenzi wake (ex), mrembo Briana nchini Australia.

 

Harmonize amefunguka kuwa, video hiyo ilikuwa ya kitambo na si kweli kwamba amechepuka hivi karibuni.

Video hiyo ni ya wimbo wake wa The Way You Are unaopatikana kwenye albam yake mpya ya Made For Us.

 

“Ni video yakitambo, iliachiwa kimakosa. Timu yangu inashughulikia jambohilo. Mwanaume mnene aliye kwenye video hiyo siyo mimi,” amesemaHarmonize.

Harmonize akiwa na mpenzi wake (ex), mrembo Briana wa nchini Australia.

Konde Boy anamsifia mchumba wake Kajala kwa kuhakikisha kuwa ana mabadiliko katika umbo lake.

“Mwili wangu una afadhali, mke wangu alinifanyia jambo, asante mpenzi wangu. Hakuna ninaloweza kufanya kuhusu mambo ya zamani,” anasemaKonde Boy.

 

Hata hivyo, Harmonize anawakejeli wapenzi wake watatu wa zamani akiwemo Briana katika wimbo wake wa My Way.

 

Katika wimbo huo, Harmonize anawashambulia wapenzi wake watatu wa zamani, Wolper, Sarah na Briana na anamsifia mchumba wake wa sasa ambaye ni Kajala.

 

Harmonize anadokeza kwamba, bado alikuwa mgeni wa mapenzi wakati alipokuwa akitoka kimapenzi na muigizaji Wolper na alitengananaye kufuatia hofu ya kushindana na matajiri.

 

“Ile mwanzomwanzo nalijuakopa, moyo ukadondoka kwa Wolper. Ningali bado mdogo nikaogopa, hivi nitawezaje kushinda navibopa,”  anasema Harmonize katika wimbo huo wa dakika mbili.

 

Harmonize anaendelea kusema kuwa, alizipuuza pesa za mwanamitindo Sarah Michelloti ambaye alikuwa mkewe kwa muda na kusema kwamba pesa zake ni karatasitu.

 

“Nikasema hasara roho pesa makaratasi, si nikampa Sarah roho kulipiza kisasi. Labda nisemeni mambo ya ujana na pengine nyota zilipishana. Kila siku tukawa tunagomba na hapa kati kabla hajaja Briana,”anasema Harmonize.

Stori; Mwandishi Wetu, Dar

#BREAKING: NDEGE ya PRECISION YAANGUKA ZIWANI BUKOBA, UOKOAJI UNAENDELEA..

Leave A Reply