The House of Favourite Newspapers

Harmonize Agawa Vitambulisho, Amwaga Mkwanja Kariakoo – Video

STAA wa muziki kutoka Lebo ya Wasafi (WCB), Harmonize ametoa vitambulisho 200 kwa wamachinga katika soko la Kariakoo, jijini Dar es Salaam na kuwamwagia pesa za kutosha ambazo haijajulikana ni kiasi gani, leo Ijumaa, Machi 22, 2019.

 

Harmonize ametoa vilivyotolewa na Rais John Magufuli, maalumu kwa ajili ya wafanyabiashara wadogowadogo, ambavyo kila kimoja huuzwa Sh20,000. Mbali na kutoa vitambulisho hivyo, msanii huyo ambaye aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sofia Mjema, ameahidi kutoa vingine zaidi kwa kila shoo atakayopata.

 

“Mimi ni mmachinga na nitaendelea kuwa machinga maisha yangu yote, ndio maana siwasahau watu mnaofanya kazi hii, nitajitahidi kuwakumbuka kadri nitakavyojaliwa ili nanyi niwainue hapo mlipo.

“Tunamshukuru Rais Magufuli kwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya kufanya biashara, kwani enzi zetu tulikuwa tukikimbizana na mgambo, kila kukicha,” alisema Harmonize.

HUZUNI: Dada MLEMAVU Aliyemkimbilia HARMONIZE Kutoka Ubungo Akamkosa!

Comments are closed.