The House of Favourite Newspapers

Harmonize Akiri Kajala Masanja Kumfanya Ashinde na Kukesha GYM Akifanya Mazoezi

0
Kajala Masanja au Mama Pau.

Harmonize au Konde Boy Mjeshi; ni supastaa wa Bongo Fleva ambaye anakiri kwamba inapotokea mhuni akampenda mwanamke mrembo, basi ni noma, IJUMAA linaripoti.

Harmonize anakiri kwamba, mwanamama Kajala Masanja au Mama Pau amemfanya ashinde na kukesha kwenye ‘gym’ akifanya mazoezi.

 

.

 

Hii ni baada ya kugundua kwamba, mwigizaji Kajala anapenda kufanya mazoezi ya gym na amekuwa akifanya hivyo kwa muda mrefu sasa tangu mwanzoni mwa mwaka jana.

Kwa mujibu wa Kajala, amefanikiwa mno kupunguza ule mwili wake mkubwa na sasa amekuwa mwepesi na mwenye mwonekano wa kuvutia.

 

HARMO AFANYA KILA LIWEZEKANALO

Sasa; baada ya kugundua hilo, Harmonize au Harmo ambaye amekuwa akifanya kila linalowezekana ili Kajala amsamehe na kurudisha penzi lao hivyo naye ameingia gym kupunguza mwili na kujiweka fiti akiamini labda mwanamama huyo atavutiwa naye na kumlegezea kamba.

 

Juu ya upendo wa Harmonize kwa Kajala, hakuna mwenye shaka kwani jamaa huyo amekuwa hapoi wala haboi ili tu kumlainisha mwanamama huyo.

Kwa mujibu wa Harmonize, sababu ya kuingia gym kwenye mazoezi ni kwa sababu ya Kajala ambaye amemvutia kuwa mtu wa mazoezi.

Konde Boy anasema kuwa, yote anayofanya ni kutokana na Kajala.

Harmonize au Konde Boy Mjeshi.

HARMO: MHUNI AKIPENDA!

“Amenifanya kuwa mtu wa mazoezi, nyie mhuni akipenda! Mwanamke wangu ndiye mshawishi wangu…” Anasema Harmonize.

Hii inaonesha ni jinsi gani penzi lake kwa Kajala limemvutia Harmonize zaidi, lakini pia ufanyaji wa mazoezi wa mwanamama huyo umemvutia jamaa ili aende naye sawasawa ili kumuonesha mapenzi ya hali ya juu aliyonayo kwake.

 

Katika kumshawishi Kajala amrudie, Harmonize amekuwa akifanya mambo kedekede ambapo mwishoni mwa mwezi Machi, aliweka bango lake na mwigizaji huyo katika eneo la Kinondoni-Manyanya jijini Dar.

Harmonize alisema bango hilo lenye maandishi ‘Lovers’ lilimgharimu shilingi milioni 12  za Tanzania.

 

“Niliweka mimi 100%. Nilitumia milioni 12. Litakuwa pale kwa takriban miezi sita,” alisema Harmonize.

Mbali na hilo, mapema mwezi Aprili, Harmonize alikwenda katika duka la vito na kutafuta cheni ya thamani ambayo Kajala alikuwa akiipenda enzi za uhai wa penzi lao.

Harmonize alisema alitumia shilingi milioni tano za Tanzania kupata cheni hiyo ya dhahabu.

“Ni tamu sana kutumia pesa zako kwa mtu unayeMpenda. Wakupeleka sasa? 5M kwa dhahabu,” alisema Konde Boy.

Kama hiyo haitoshi, hivi karibuni Harmonize alinunua picha ya ex-wake huyo na kuitundika kwenye chumba chake cha kulala.

 

Harmonize alisema alifikia hatua hiyo ili kila asubuhi anapoamka awe anakutana na sura ya mwigizaji huyo.

“Wewe ndiye mtu pekee nitakuona nikifungua macho yangu kila siku. Tafadhali rudi. Tabasamu kwa ajili yangu popote ulipo!!…Nirudie tena,” alisema Harmonize.

 

Pia Aprili 13, mwaka huu, Harmonize alitangaza kumnunulia Kajala gari la kifahari aina ya Range Rover na kudai kuwa hilo ndilo gari la ndoto zake.

 

Harmonize alisema anataka Kajala ajue kwamba anayajuta sana maovu aliyomtendea pamoja na familia yake hadi kusababisha kuvunjika kwa uhusiano wao.

 

“Ninaeleza majuto ya yote niliyokufanyia!!!! Ninachoomba kwako ni msamaha wa dhati wa moyo wako!!!! Frida (Kajala) wewe ni mtu wa Mungu sanaa!!! Unasali, pia bila shaka unatambua hakuna mkamilifu, hutakuja kuanza upya mama. Unanifahamu zaidi, rudi tena. Usisahau mimi ni mtoto wa masikini mwenzio tu. Nina familia, wajomba, shangazi, wadogo na ndugu kibao maskini ambao nikifa leo ndiyo watakaonizika, ila nimeona wewe ndiye unastahili,” aliandika Harmonize.

 

Gari alilonunua Harmonize, badala ya kuwekwa namba ya usajili, limewekwa jina la Kajala 1 GP kuashiria kwamba alinunua maalum kwa ajili mwigizaji huyo ambaye alidumua naye kwa miezi michache tu.

 

Mbali na kununua zawadi za thamani, Harmonize pia amekuwa akimwomba msamaha hadharani mama huyo wa Paula Kajala.

 

Harmonize na Kajala waliachana kwa sababu ya ile skendo ya ‘washa taa’ ambapo jamaa huyo alidaiwa kutaka kula kuku na mayai yake baada ya kumtaka kimapenzi Paula akiwa ni mpenzi wa msanii Rayvanny.

Stori; Khadija Bakari, Dar

Leave A Reply