The House of Favourite Newspapers

Harmonize Amponza Jane Misso

0

MWANAMAMA anayeimba Nyimbo za Injili, Jane Misso amekiri kuponzwa na wimbo alioimba na staa wa Bongo Fleva, Harmonize.

Jane Misso ambaye ni Mkristo anasema kuwa, baada ya kutoa Wimbo wa Omoyo Remix akishirikiana na Harmonize ambaye ni Muislam, baadhi ya watu wamemtenga.


“Tunatofautiana sana uwelewa na
siyo makanisa yote yamenitenga, kuna wengine mbona wame-support, maaskofu wengi, wachungaji wengi wamefurahia sana, wamefurahi mno, kitu ambacho sikutegemea, lakini wengine wameonekana kukwazika na hata kuna wengine nilikuwa na safari zangu kuelekea sehemu f’lani wamesema wame-cancel, lakini mimi sishangai,” anasema Jane Misso.


Anasema kuwa, anawapa muda
wanaohoji kwa nini ameamua kuimba na Harmonize akisema hata Yesu alijichanganya na wenye dhambi hivyo hajaona kama kuna tatizo.


Jane Misso anammwagia misifa
kama yote Harmonize kwa kusema kuwa ni kijana mwelewa, mnyenyekevu na mwenye heshima na ndiyo maana hakusita kufanya naye kazi kwani alijua nia yake ni nzuri.


Hadi sasa, wimbo huo una watazamaji
zaidi ya milioni 1.7 ukiwa unashika nafasi ya pili kwenye Mtandao wa YouTube.

STORI; SIFAEL PAUL, DAR

Leave A Reply