The House of Favourite Newspapers

Harmonize Atabiriwa na Mashabiki wa Muziki Kumfunika Diamond

0
Harmonize akiwanampenzi wake Kajala.

 

Baadhi ya mashabiki wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Tanzania wanatabiri kwamba, wasanii Harmonize au Konde Boy na Rayvanny ndiyo walio kwenye nafasi ya kufanya udhubutu wa kufikia au kufunika utajiri na mafanikio ya msanii Diamond Platnumz katika muziki.

 

Mchambuzi wa masuala ya burudani nchini Tanzania, Hope Tyga anasema kwamba kwa sasa, Diamond au Mondi ndiye msanii tajiri namba mbili katika Ukanda wa Afrika Mashariki, nyuma ya msanii na mwanasiasa Bobi Wine wa Uganda.

 

Kwenye listi hiyo, mshindani wa Diamond wa muda wote kimuziki, King Kiba anashika namba sita huku Harmonize akiwa namba nane.

 

Kwa mujibu wa jamaa huyo, itakuwa ni vigumu mno kwa wasanii wengine katika vizazi vijavyo kufikia hatua ambazo Diamond amefika, lakini Harmonize na Rayvanny wana nafasi kubwa ya kumfikia kwa kile anachosema kwamba wapo katika mkondo mzuri kama wataendelea kukaza buti.

 

Msanii Diamond Platnumz.

“Ni vigumu sana wasanii wengine kufika level za Diamond. Wasanii ambao kidogo kwa hapo baadaye wanaweza kufikia utajiri wa Diamond ni Harmonize au Rayvanny maana wana misingi mizuri, ila wengine itakuwa vigumu sana,” anasema Hope.

 

Anasema kuwa, kigumu ambacho kinawakwamisha wasanii wengine ni kushindwa kujiuza vizuri kibiashara kama ambavyo Diamond anafanya na wengi hujikita katika misingi ya kufanya muziki wa kufurahisha na kuburudisha ilihali Diamond anachukulia muziki kama biashara yake kuu.

 

“Njia alizopita Diamond wengi hawapiti, wasanii hawajui kuji-brand kibiashara. Kilichomtajirisha Diamond ni branding. Ame-brand vizuri neno Wasafi ndiyo maana amepata business partners (wabia).

 

“Kwa asilimia kubwa utajiri wa Diamond umetokana na biashara ya lebo na media. Wasanii wengi wamekaa kizembe mno, hawana akili ya biashara, wanawaza kupata lakilaki za show,” anasema jamaa huyo.

 

Anawasifia baadhi ya wasanii ambao wamejiweka katika mkondo mzuri kibiashara na kutumia umaarufu wao vizuri ili kujiongezea kipato kando na muziki.

 

“Kwa sasa pongezi kubwa ziende kwa Diamond, Jux, Vanny, Harmo hawa wanajua kujiongeza,” anamalizia.

Stori; Khadija Bakari, Dar

Leave A Reply