The House of Favourite Newspapers

Smith Amponza Mwakinyo, Afungiwa Uingereza, Apanda Viwango Kwa Nafasi Mbili Duniani

0
Hassan Mwakinyo.

 

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo amesimamishwa kucheza pambano lolote nchini Uingereza na bodi ya udhibiti ya mchezo wa ngumi nchini huo BBBC kwa kipindi kisichojulikana tangu apoteze pambano lake dhidi ya Liam Smith mapema mwezi huu nchini humo.

 

Licha ya bodi hiyo kutoweka wazi sababu za kumfungia Mtanzania huyo ni wazi imetokana na matokeo ya kushangaza katika pambano lake lililopita nchini humo kufuatia kushindwa kuendelea kwa madai ya kuwa amepata enka iliokuwa imetokana na viatu alivyokuwa amepewa kucheza pambano hilo lilifanyika kwenye Ukumbi wa M & S Bank Arena uliopo Liverpool nchini humo.

 

Hata hivyo bodi hiyo haijaweka wazi katika mtandao wa kuhifadhi kanzi data za mabondia kuwa kifungo hicho kitakuwa cha muda gani licha ya kuwepo kwa taarifa za pambano la marudiano ambazo zilitolewa na Hassan Mwakinyo baada ya siku chache tangu apoteze pambano hilo.

 

Kifungo hicho hakiwezi kumzuia bondia huyo kucheza pambano lolote katika mataifa mengine isipokuwa ndani ya taifa la Uingereza pekee huku akiwa amepanda viwango kwa nafasi mbili kutoka ya 40 duniani hadi ya 38 katika mabondia 1953 wa uzani wa super walter.

NAY ALIAMSHA DUDE FIESTA, AVAMIWA na MASHABIKI STEJINI, WALINZI WASHINDWA KUWAZUIA, VAIBU LA KUTOSHA

Leave A Reply