The House of Favourite Newspapers

Video: Harmorapa, Juma Nature, Msaga Sumu Kuandika Historia Sikukuu ya Pasaka – Dar Live

0


MKALI asiyeshikika katika Muziki wa Hip Hop Bongo, Juma Kassim ‘Nature’ na Harmorapa wanatarajiwa kulivuta Jiji la Dar Sikukuu ya Pasaka ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uli­opo Mbagala-Zakhem.

Akiwatambulisha wakali hao leo mbele ya vyombo vya habari, Meneja na Mratibu wa Dar Live, Juma Mbizo al­isema kuwa, mashabiki wengi wame­kuwa na hamu ya kushudia wakali hao wakipanda juk­waa moja na kulisimamisha kama wa­fanyavyo kwenye matamasha mengine.

“Tumesikia kilio cha mashabiki na tu­mewafikia, Nature, Harmorapa usiku huo atatoa shoo ya mperampera kwa kugonga nyimbo zake kuanzia Mgambo, Inaniuma Sana hadi Mtumba,” alisema Mbizo huku Harmorapa akikinukisha kwa ngoma zake mpya ikiwemo aliyoiachia hivi karibuni, Kiboko ya Mabishoo.

Mbizo alionge­za kuwa mbali na wakali hao, wakali wengine watakaokimbiza ni fundi wa Mziki wa Uswazi ‘Singeli’, Msaga Sumu, MC Darada pamoja na Dula Makabila.

“Pia tutakuwa na msanii gumzo kila kona, Harmorapa wakali wa Singe­li, Dulla Makabila na Msaga Sumuna wengine wengi,” alisema Mbizo.

Mapema kuanzia asub­uhi kutakuwa na burudani na michezo mingi kwa watot o itakayoon­gozwa na Kundi la Makhirikhiri kutoka Tanzania.

Kwa upande wake Haromrapa ameahidi kuweka historia ya burudani ndani ya Dar Live huku akiwahakikishia mashabiki wake kuwapa kile wanachostahili.

Msaga Sumu, Darada na Dula Makabila wametamba kufanya maajabu kwenye shoo hiyo, huku wakiwaomba mashabiki zao wajitokeze kwa wingi kwani DAR LIVE ndiyo kiwanja pekee watapata Burudani ya kiwango.

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe nisiasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaa, muziki na nyingine kali zikufikie kwa wakati.

Leave A Reply