The House of Favourite Newspapers

Harnaaz Mrembo wa India Taji la ‘Miss Universe’

0

MREMBO Harnaaz Sandhu kutoka nchini India ameibuka mshindi kwenye mashindano ya ulimbwende ya ‘Miss Universe’ siku ya jana Desemba 12, 2021 huku akiwatoa jasho washiriki wengine 80 kutoka mataifa tofauti duniani.

 

Mashindao hayo yalipambwa kwa maonesho tofauti tofauti ya mavazi yaliyopangwa kulingana na mila na desturi za kadhia tofauti tofauti. Mwaka jana mrembo kutoka nchini Mexico alitwaa taji hilo kwa kuonesha vazi la asili kutoka nchini Israel.

 

Warembo hao walipita jukwaani wakiwa wamevalia mavazi ya ufukweni, utamaduni, kitaifa, mavazi ya usiku maarufu kama evening gowns pamoja na hayo pia waliulizwa maswali ya papo kwa papo yaliyolenga kupima uelewa na utashi wao wa kupambanua mambo tofauti tofauti.

Leave A Reply