The House of Favourite Newspapers

Kane Kutua Madrid, Sanchez West Ham, Lingard Kuondoka Man U?

0

KLABU ya Barcelona wanataka kumsajili mshambuliaji wa Argentina Lautaro Martinez, 22, kutoka klabu ya Inter Milan lakini wanakabiliana na ushindani mkali kutoka kwa Real Madrid na Manchester City. (Marca).

 

Klabu ya Wolves haitamuuza Adama Troare, 24, kwa dau lolote chini ya pauni milioni 70 huku winga huyo akihusishwa na mipango ya kuhamia Liverpool. (Football Insider).

 

Arsenal wanalenga kumsajili beki wa Athletic Bilbao Unai Nunez, 23, kama kipaumbele chao kwa usajili wa majira ya kiangazi. Beki huyo wa Hispania ana kifungu cha mkataba kinachoelekeza kuuzwa kwa euro milioni 30. (La Razon – in Spanish).

 

Shirikisho la mpira duniani (Fifa) linapanga kuongeza muda wa moja kwa moja wa msimu wa 2019-20 ili kuruhusu kila nchi kuamua ni lini msimu huo utaisha. (The Athletic – subscription required).

 

Liverpool, Manchester City na Manchester United wote wameonyesha nia ya kumsajili winga wa Hispania na Valencia Ferran Torres, 20. (Goal).

 

Kiungo wa Manchester United Jesse Lingard, 27, hana mpango wa kuihama klabu hiyo mwishoni mwa msimu. Kiungo huyo anahusishwa na uhamisho kuelekea Arsenal na Everton. (Metro).

 

Liverpool wanakusudia kutuma ofa mbili za usajili kwa kiungo wa Uswizi Denis Zakaria na mshambuliaji wa Ufaransa Marcus Thuram wote kutoka klabu ya Borussia Monchengladbach. (Express).

 

Mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud, 33, amefanya mazungumzo ya awali juu ya kuongeza mkataba katika klabu ya Chelsea. (Football.London).

 

Chelsea pia inajipanga kushindana na Arsenal katika mbio za kumsajili beki yaw a Ujerumani Jerome Boateng, ambaye anakaribia kuingia katika miezi 12 ya mwisho ya mkataba wake na klabu ya Bayern Munich. (Mail).

 

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya England Jadon Sancho, 20, amekataa uhamisho wa kuelekea Manchester United mwisho wa msimu huu iwapo watashindwa kufuzu katika michuano ya klabu bingwa (Sun).

 

Real Madrid inataka kumsaini mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane mwenye umri wa miaka 26. (Sport).

 

Leicester, Newcastle, Crystal Palace na Aston Villa wana hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Rangers na Colombia Alfredo Morelos, 23. (Talksport).

 

West Ham imekuwa ikiwasiliana na wakala wa mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez huku wakifikiria kumsaini mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal na Manchester United.

 

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 kwa sasa anahudumu kwa mkopo katika klabu ya Inter Milan kutoka Man United. (Sport Witness).

 

Kiungo wa kati wa Manchester City na Hispania David Silva, 34, huenda akapatiwa mechi ya mwisho ya kumuaga katika uwanja wa Etihad mwisho wa msimu iwapo mlipuko wa coronavirus utamzuia kuwaaga mashabiki wa klabu hiyo baada ya kuichezea klabu hiyo kwa miaka 10 kitu ambacho kimemsaidia kushinda taji la ligi kuu mara. (Mail).

 

Aliyekuwa mshambuiaji wa Manchester United na Tottenham Dimitar Berbatov anaamini kwamba mshambuliaji wa klabu ya RB Leipzig na Ujerumani Timo Werner, 24, atafurahia kujiunga na Bayern Munich badala ya Liverpool mwisho wa msimu huu . (Mirror).

 

Leicester, Tottenham na Everton wote wana hamu ya kumnunua kiungo wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 25 Baptiste Santamaria, ambaye anaichezea klabu ya Angers katika ligi ya daraja la kwanza ya Ufaransa. (Express).

 

Klabu za ligi ya Premia zimenunua vifaa vyao vya kupima virusi vya corona huku kukiwa na hofu kwamba mechi zitachezwa bila mashabiki. (Star).

 

Beki wa Uholanzi na Manchester United Timothy Fosu-Mensah, 22, anakabiliwa na hali ya switofahamu katika klabu hiyo huku mkufunzi Ole Gunnar Solskjaer akifikiria iwapo anaweza kumuongezea mwaka mmoja katika kandarasi yake (Mirror).

 

Mshambuliajhi wa Celta Vigo na Urusi Fedor Smolov, 30, alikiuka hatua ya Uhispania kuweka sheria ya kutotoka ndani , akiwa ni mchezaji wa pili wa taifa hilo kwenda kinyume na sheria hiyo kwa kurudi nchini mwake. (AS, in Spanish).

Leave A Reply