The House of Favourite Newspapers

Corona: Waziri Mkuu Uingereza Yuko Chumba cha Mahututi

0

WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, amepelekwa katika chumba cha kuhudumia wagonjwa mahututi baada ya hali yake kiafya kuwa mbaya kwa siku kumi zaidi kwa sababu ya ugonjwa wa virusi vya Corona, kwa mujibu wa msemaji katika makazi ya Waziri Mkuu.

 

Johnson amemuambia waziri wa mambo ya nje, Dominic Raab, kuchukua usukani “pale ambapo kutakuwa na ulazima wa kufanya hivyo”, msemaji ameongeza.

 

Waziri mkuu huyo mwenye umri wa miaka 55, alilazwa katika hospitali ya St Thomas mjini London wakati hali yake ya kiafya ilipokuwa haina ahueni huku homa na kukohoa kukiongezeka zaidi siku ya Jumapili. Hatua hiyo imechukuliwa baada ya ushauri kutoka kwa timu yake ya matibabu na anaendelea kupata huduma stahiki.

 

Taarifa zaidi zinaarifu kuwa:  “Tangu Jumapili jioni, Waziri huyo Mkuu amekuwa chini ya madaktari wa hospitali ya St Thomas mjini London, baada ya kuonyesha dalili mbaya za virusi vya Corona.

 

“Mchana wa leo, hali ya Waziri Mkuu hali ya afya yake imezidi kuzorota na kutokana na ushauri uliotolewa na timu yake ya madaktari, amehamishwa hadi kitengo cha wagonjwa mahututi hospitalini humo.”

 

Mapema Jumatatu ujumbe uliandikwa kwenye mtandao wa Twitter ukiashiria kwamba anaendelea kupata afueni.

 

Matukio ofisi ya waziri mkuu na maambukizi ya Virusi vya Corona mpaka sasa:

Machi 10: Waziri wa afya Nadine Dorries alikuwa mbunge wa kwanza kupima virusi vya ugonjwa huo, muda mfupi baada ya kuhudhuria mapokezi ya Mtaa wa Downing.

Machi 27: Waziri mkuu Boris Johnson na Katibu wa Afya Matt Hancock wote wawili wakaachia video zao kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter wakisema wana uambukizo wa corona na wanajitenga. Saa kadhaa baadaye , afisa mkuu wa matibabu Profesa Chris Whitty alifichua kuwa alikuwa akijitenga na dalili.

Machi 30: Mshauri mkuu wa waziri mkuu Dominic Cummings naye aliarifiwa kujitenga binafsi na uambukizo wa virusi hivyo

Aprili 2: Matt Hancock anarudi kazini baada ya watu saba kufa wakati alipokuwa kwenye karantini akiwa na ahueni kubwa.

Aprili 3; Boris Johnson aachia video akiwa kwenye ghorofa yake ya Namba 11 akisema anaendelea kujitenga kwani bado anapata homa na inapanda.

Aprili 4: Carrie Symonds, ni mchumba wa waziri mkuu Boris ambaye kwa sasa ni mjamzito,  naye amekuwa akijitenga katika chumba chake huko Camberwell.

Aprili 5: Waziri mkuu apelekwa hospitalini ‘kwa tahadhari’.

Aprili 6: Ofisi ya waziri mkuu yakataa kutoa taarifa wazi zaidi kuhusu hali yake na msemaji wake asema bado ana kikohozi cha ‘kuendelea’ na joto mwilini

Aprili 7; Waziri mkuu Boris Johnson ahamishiwa chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya St Thomas na nafasi yake kukaimiwa na waziri wa mambo ya nje Dominic Raab.

Leave A Reply