The House of Favourite Newspapers

Haruna Niyonzima: Msinifananishe Na Chama

Haruna Niyonzima

HARUNA Niyonzima amesikia namna ambavyo mashabiki wa Simba wanavyosema kiungo mpya, Mzambia Claytous Chama ni bora zaidi yake akawajibu.

 

Chama ambaye amesa­jiliwa Simba hivi karibuni kwa thamani ya Sh mil 70 alionyesha uwezo mkubwa katika mchezo wa Simba Day dhidi ya Asante Ko­toko ya Ghana na kuwa­fanya mashabiki wa timu hiyo wadai ameziba pengo la Niyonzima aliyejiunga na kikosi hicho msimu uli­opita kwa Sh Mil 90.

 

Niyonzima hajajiunga na Simba tangu ilipomalizika michuano ya SportPesa Juni mwaka huu nchini Kenya huku kukiwa na taarifa kuwa anataka ku­vunja mkataba na timu hiyo kutokana na baadhi ya vitu kukiukwa.

Mzambia Claytous Chama.

Niyonzima amezungumza na Championi Juma­mosi kuhusiana na Chama kuonekana bora zaidi yake; “Chama amekuja Simba kama wachezaji wengine wote, yeye ana staili yake ya uchezaji na mimi nina staili yangu ya uchezaji, watu wasilete mgongano kati yetu, kwani iwapo nitamzungumzia basi inaweza kuleta uto­fauti ndani ya timu.”

 

“Mimi nina CV yangu katika mpira wa nchi hii, Chama amefanya nini? Kwa sasa sitaki watu wanilinganishe nae kwa kuwa najua wote ni wachezaji na tutakuja kucheza wote na kuisaidia timu, wengi wame­kuwa wakinihoji juu ya uwezo wake, mwalimu ndiye anayeweza kum­zungumzia zaidi.

 

“Chama ni mchezaji kama ilivyo kwa wachezaji wengine ameku­ja kuitumikia Simba, mimi nitapata nafasi na yeye atapata nafasi,” alisema Niyonzima ambaye aliwahi kuwika na Yanga.

Comments are closed.