The House of Favourite Newspapers

Takukuru: Tanzania Yafanya vizuri katika mapambano dhidi ya rushwa kwa mwaka 2023

0
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), Salum Hamduni.

Mapambano dhidi ya rushwa yameendelea kuimarika nchini ambapo Tanzania imepanda kwa nafasi saba juu katika mapambano dhidi ya rushwa kwa mujibu wa taarifa ya Transparency International ya mwaka 2023 iliyotolewa Januari 30 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), Salum Hamduni, Tanzania imepata alama 40 kati ya alama 100 na hivyo kupanda hadi nafasi ya 87 mwaka 2023, kutoka alama 38 mwaka 2022 ambapo ilikuwa nafasi ya 94.

“Hii inamaanisha kuwa Tanzania imefanya vizuri katika mapambano dhidi ya rushwa kwa mwaka 2023 ikilinganishwa na mwaka 2022,” amesema Hamduni.

Ameongeza kuwa taarifa hiyo inaonesha kwamba Tanzania ni moja kati ya nchi 28 duniani zinazoonesha kuimarika katika kipindi cha mwaka mmoja na pia ni miongoni nchi sita kati ya nchi 180 zilizofanyiwa tathmini kuonesha kuimarika katika kupungua kwa vitendo vya rushwa kwa wastani mzuri.

Kwa miaka 10 mfululizo Tanzania imekuwa ikipanda katika viwango vya kudhibiti rushwa.

Mkurugenzi Mkuu huyo wa TAKUKURU alikuwa akitoa taarifa ya utendaji kazi ya TAKUKURU kwa mwaka 2022/2023 Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma.

Leave A Reply