Hati ya Kumkamata Wema Yaibua Utata Kortini

staa wa filamu Bongo

Hati ya kumkamata staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu iliyotolewa jana na shahidi wa serikali katika kesi ya kukutwa na madawa ya kulevya, iliibua utata baada ya wakili wa mshtakiwa huyo kuikataa huku mwanasheria wa serikali akiikubali.

 

Hiyo ilikuja baada ya wasilisho la pingamizi lililotolewa na wakili wa utetezi, Peter Kibatala, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kwamba kielelezo kilichowasilishwa na Shahidi upande wa utetezi, ambaye ni ofisa wa ofisi ya Mkuu wa Upelelezi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Inspekta Willy kina mapungufu ya kisheria, hivyo kisipokelewe.

staa wa filamu Bongo

Katika hoja zake, wakili wa serikali, Constantine Kakula, amedai kuwa hati hiyo ipo sahihi, hivyo ipokelewe na Mahakama. Kutokana na maelezo hayo Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 4, mwaka huu kwa ajili ya kutoa uamuzi.

 

Mbali ya Wema, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas ambao wote wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kutumia dawa za kulevya.

NA DENIS MTIMA/GPL


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment