The House of Favourite Newspapers

HATIMAYE GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMISI LATINGA MTAANI – PICHAZ

Wafanyakazi wa Global Publishers wakiongozwa na Meneja wao Mkuu, Abdallah Mrisho (kulia mwenye miwani) wakiwa mtaani maeneo ya Morocco wakiuza Gazeti la Spoti Xtra.

TIMU nzima ya wafanyakazi wa Global Publishers, wakiongozwa na Meneja Mkuu, Abdallah Mrisho, mapema leo wametinga mtaani kulinadi gazeti la Spoti Xtra ambalo ni jipya na ambalo limekuwa likiingia mtaani siku za Jumaili  na sasa limeanza kuingia mtaani kila siku ya Alhamisi kwa bei ya shilingi 500.

Abdallah Mrisho akimuuzia Gazeti Spoti Xtra mteja ambaye pia ni kondakta wa daladala Stendi ya Makumbusho.

Akizungumzia ujio huo wa gazeti hilo la Spoti Xtra kila Alhamisi, Mrisho amesema lengo kubwa ni kumaliza kiu ya wapenzi wa habari za michezo na ndiyo sababu kubwa ya kuliingiza mtaani siku hiyo.

Mhariri Kiongozi wa Global Publishers, Amran Kaima (kulia) na mwandishi wa michezo, Lucy Mgina (kushoto) wakimpa zawadi ya tisheti na kofia venda aliyekuwa akiuza Gazeti la Spoti Xtra maeneo ya Morocco.

Wasomaji wa gazeti la Spoti Xtra ambao walichangamka kulinunua maeneo ya Stendi ya Makumbusho na maeneo ya makutano ya mataa ya Morocco-Kinondoni, wamelipongeza kwa mwonekano mzuri na kwa namna ambavyo limesheheni habari za michezo.

Wafanayakazi wa Global Publishers wakiwa katika picha ya pamoja na mavenda na wateja wao.

“Kiukweli nyie watu wa Global mmetusaidia sana kuliingiza gazeti hilo siku ya Alhamisi kwani tumekuwa tukikosa habari za michezo na kubaki tukitafakari nini cha kufanya, hongereni sana,” alisema  mmoja wa madereva wa stendi ya makumbusho aliyejitambulisha kwa jina la Masudi Khamis.

Hawa ni wafanyakazi wa Global Publishers wakiongozwa na Meneja wao Mkuu, Abdallah Mrisho (kulia) wakiwa mtaani kuuza Gazeti Bora la Michezo nchini, SpotiXtra.

 

Mfanyakazi wa Global Publishers, Samwel Shigongo akimuuzia Spoti Xtra kondakta wa daldala.
Mrisho akimuuzia Spoti Xtra mteja wake.

 

PICHA NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

Kishindo cha Gazeti la Sport Xtra Chatikisa Jiji

Comments are closed.