The House of Favourite Newspapers

Chama Akabidhiwa Waarabu Ligi ya Mabingwa Afrika

0

KUTOKANA na kasi aliyoanza nayo kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy akitokea benchi, kuna uwezekano mkubwa wa Kiungo wa Simba, Clatous Chama akaanza kikosi cha kwanza Jumamosi dhidi ya Wydad Casablanca.

Chama alitimiza majukumu yake kwa umakini dakika 28 alizozitumia dhidi ya Jwaneng Galaxy alipochukua nafasi ya Willy Onana.

Ikumbukwe kwamba, huo ulikuwa ni mchezo wa kwanza kwa Kocha Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha, Desemba 2, ubao uliposoma Jwaneng Galaxy 0-0 Simba. Huenda akapewa nafasi ya kuanza kwenye mchezo dhidi ya Waarabu wa Morocco, Wydad Casablanca.

Kuingia kwa Chama kwenye mchezo huo kuliongeza kasi eneo la wapinzani huku pasi zake zaidi ya 11 alizotoa akitumia mguu wa kulia zikifika kwa wahusika na alipiga shuti moja ambalo liligonga mwamba dakika ya 90.

Benchikha aliweka wazi kuwa, hatatumia majina makubwa kwenye upangaji wa kikosi cha kutafuta ushindi bali kila mchezaji atakayeonesha kazi kubwa uwanjani atapewa nafasi.

“Kila mchezaji ana nafasi ya kufanya vizuri na kuwa kwenye kikosi cha kwanza, hivyo hakuna mwenye nafasi kikosi cha kwanza, kila mmoja ana nafasi kuanza, akionesha uwezo atapata nafasi,” alisema Benchikha.

STORI NA LUNYAMADZO MLYUKA

KUTOKA GHANA: ALI KAMWE AKISHUHUDIA TIZI LA MWISHO – ”WACHEZAJI WAPO TAYARI”…

Leave A Reply