The House of Favourite Newspapers

Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi Abadili Mfumo leo dhidi ya Medeama

0
Miguel Gamondi.

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi, unaweza kusema amejipata baada ya kubadilisha mfumo wake kutoka kutumia mabeki wa kati wawili na kuanza kutumia mabeki watatu wa kati jambo ambalo limeanza kuzaa matunda ndani ya timu hiyo.

Mfumo huo ulionekana katika mchezo dhidi ya Al Ahly ambapo Gamondi alionekana kuwatumia mabeki Ibrahim Bacca, Bakari Mwamnyeto na Dickson Job tofauti na mchezo wa kwanza dhidi ya CR Belouizdad ambapo aliwatumia Dickson Job na Ibrahim Bacca pekee.

Yanga katika mchezo dhidi ya Al Ahly baada ya Gamondi kubadilisha mfumo huo, ilimsaidia na kujikuta akitoa sare ya bao 1-1 tofauti na mchezo ambao aliwatumia mabeki wawili wa kati ambapo alipoteza kwa kufungwa mabao 3-0.

Kuelekea katika mchezo wa leo Ijumaa dhidi ya Medeama, taarifa ambazo limezipata Spoti Xtra ni kwamba, Kocha Gamondi amenogewa na mfumo huo mpya ambao inaelezwa ataendelea kuutumia.

“Kocha Gamondi ameonekana kunogewa na mbinu ya kuwatumia mabeki watatu wa kati na inaweza kuendelea katika mchezo wetu unaofuata dhidi ya Madema kwani hata mazoezini amekuwa akiwachezesha pamoja mabeki hawa na kuwapa maelekezo ya kutosha,” kilisema chanzo hicho.

Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, alisema: “Hayo ni mambo ya kiufundi, anatakiwa kuyaelezea mwalimu kuhusu kubadili mbinu na timu itacheza vipi kwa upande wetu niweze kusema tunahitaji matokeo ya ushindi dhidi ya Madeama kuliko kitu chochote, hivyo tunakwenda kuhakikisha tunapambana kwani sio rahisi, lakini itabidi tujitahidi kwa hilo.”

Leave A Reply