HATIMAYE ROONEY ATOKA KIFUNGONI

WAYNE Rooney juzi alionekana akiendesha gari kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka miwili, kwa kuwa alikuwa amefungiwa kuendesha.

 

Rooney ambaye sasa ni kocha mchezaji wa Derby County inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza England (Championship), alifungiwa kuendesha na mahakama baada ya kupatikana na hatia ya kuendesha akiwa amelewa mwaka 2017.

 

Rooney, tajiri mwenye magari mengi ya kifahari ya kila aina, licha ya kujaza ndinga kibao nyumbani kwake, hakuwa na uwezo wa kuendesha gari kwa miaka miwili.

 

Wenzetu wanazingatia sana sheria ya Drive Under Influence (DUI), yaani kuendesha ukiwa na kiwango kikubwa cha kilevi.

Sasa juzi, Rooney alionekana akiwa na shauku ya kuendesha alipokuwa akitinga kwenye gari lake la kifahari la Land Rover Overfinch lenye thamani ya pauni 219,000 (Sh milioni 656).

 

Rooney, 34, inasemekana ametoka Marekani ambako alikuwa akicheza DC United na kutua Derby kwa ushawishi wa mkewe baada ya mwanasoka huyo kupigwa picha akitoka hotelini Vancouver akiwa na mrembo saa 11:30 asubuhi.

 

Ulitokea mtifuano mkali kati yake na mkewe ambaye alisema kama wanataka kuokoa ndoa yao basi warudi England.


Loading...

Toa comment