The House of Favourite Newspapers

HATIMAYE TFF WATOA NGAO MPYA KWA SIMBA

0
Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas akionyesha ngao hiyo.

HATIMAYE Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limefanya marekebisho katika Ngao ya Jamii ambayo timu ya Simba ilikabidhiwa baada ya kuifunga Yanga, Jumatano iliyopita.

 

Alfred Lucas akizungumza jambo.

Awali Ngao hiyo ilikosewa katika neno SHIELD, Simba walikabidhiwa lakini baada ya makosa kuonekana, TFF waliomba radhi kesho yake kisha kuwaambia Simba wairejeshe Ngao hiyo kwa ajili ya marekebisho ya neno hilo.

Alfred Lucas akizungumza jambo.

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas ameionyesha Ngao iliyorekebishwa kwa waandishi wa habari leo Jumanne kwenye ofisi za shirikisho hilo, Karume jijini Dar.

Alfred Lucas akionyesha ngao hiyo.

 

NA MUSA MATEJA | GPL

Leave A Reply