Haya Mambo ya Kujiondolea Kizazi ni Kumjaribu Mungu

KATIKA hali ya kushangaza, wakati watu wanahangaika kutafuta kizazi, kusaka watoto, mwanadada aliyefahamika kwa jina la Priyanka Ramgoolam (25) ambaye kitaaluma ni daktari wa binadamu ameamua kuondoa kizazi chake jambo ambalo limeushangaza ulimwengu.
Priyanka anasema binafsi hataki kabisa kuzaa na kuitwa mama katika maisha yake hivyo kutimiza lengo lake hilo amefanyiwa upasuaji ili kuiondoa mirija yake ya uzazi(fallopian tubes) asije kubeba mimba hata kwa bahati mbaya.
Hajaolewa na hajawahi kuzaa. Amesema baada ya kufanyiwa upasuaji kuondoa mirija yake ya uzazi kwasasa ana furaha zaidi isiyo na kifani.

