The House of Favourite Newspapers

Mjadala Juisi ya Miwa Kuwa na Sumu

0

WAKATI juisi ya miwa ikionekana kupendwa zaidi Utafiti wa awali uliyofanywa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Sayansi ya Afya (Cuhas) umesema kwenye juisi ya miwa jijini Mwanza umebaini uwepo wa bakteria aina ya Escherichia Coli anayepatikana kwenye taka mwili za mfumo wa chakula wa binadamu.

 

Mtafiti wa vimelea vya magonjwa na magonjwa ya kuambukiza kutoka Cuhas, Profesa Jeremiah Seni alisema utafiti huo ulihusisha uchunguzi wa kimaabara katika sampuli 120 zilizochukuliwa kutoka kwa wauza juisi 24 jijini Mwanza na kati ya hizo sampuli 71 zilikutwa na bakteria huyo.

 

Kuupinga utafiti wanasema lazima na wewe uje na utafiti wako ndiyo maana sitaki kupiinga lakini “nahoji.”

Ni kwa kiasi gani utafiti huo uaminike kwa sababu kwanza umechukua sampuri chache na unakanganya kuhusu majibu yake kuwa kadiri walivyokuwa akichunguza waligundua kuwa vimelea hao walikuwa wanapungua kwenye juisi hiyo kila siku.

 

“Uwepo wa bakteria ulionekana kupungua kutoka asilimia 87.5 kwenye sampuli 24 zilizopimwa siku ya kwanza hadi asilimia 45.8 siku ya tano na ya mwisho wa utafiti. Hii ni ishara kuwa kupitia elimu ya ubora na usalama tunaweza kumaliza tatizo hili,” alisema Profesa Seni.

 

Wakati utafiti huu unatolewa ni wazi kuwa kulikuwa na watu walikuwa akiendesha maisha yao kupitia biashara hii, leo hii biashara yao haiaminiki tena na wateja wanaonekana kuanza kuogopa kunywa “sumu”.

 

Kibaya zaidi katika akili ya kawaida tu inaonesha kuwa, juisi inaweza kuwa isiwe tatizo lakini mazingira ya uandaaji wake na maji yanayotumika pamoja na usafi wa mazingira linaweza kuwa tatizo kubwa zaidi kuliko juisi yenyewe.

 

Maana hatujawahi kuambia kuwa miwa ina vimelea; kama leo tunaambiwa kuna taka sumu bila shaka kuna sehemu zitakuwa zinatoka.

Yawezekana kwenye maji machafu kama tuonavyo kwenye magonjwa ya kuhara.

Ushauri wangu kwa serikali ni kujitokeza haraka kuufikisha mwisho utafiti huu ulioitwa wa “awali” ili mbivu na bichi zijulikane.

 

Hakuna sababu ya kuacha taharukia katika mambo ambayo yanahusu afya ya watu; kama juisi hii ni sumu ipigwe marufuku na ikiwa siyo watu waachwe waendelee kupoza makoo yao huku wakiamini kuwa juisi hiyo inasafisha figo.

@manyota_rich #0714 895 555

Leave A Reply