The House of Favourite Newspapers

Mpaka Home: Haya Ndiyo Maisha Halisi ya Yusuf Mlela

0

 

KAMA kawa, kama dawa, kila Jumamosi katika safu hii ya Mpaka Home tunakuletea maisha ya staa mmoja wa Kibongo anapokuwa kinyumbani zaidi nje ya fani yake.

Wiki hii Mpaka Home imetinga nyumbani kwa staa wa kiume wa sinema za Kibongo, Yusuf Mlela anayeishi Kinondoni B jijini Dar.

Safari ya Mpaka Home ililenga kuona kazi au mambo anayoyafanya Mlela kwa siku nzima, akiwa nyumbani kwake hapo, jambo ambalo ilifanikiwa baada ya kumkuta mwigizaji huyo katika mazingira nadhifu kabisa.

 

 

Mpaka Home: Mlela mambo vipi? Hongera kwa mazingira mazuri ya nyumbani kwako.

Mlela: Poa na asante sana, karibu home sweet home.

Mpaka Home: Unaishi na nani hapa?

Mlela: Ninaishi na mwanangu Mwantumu na mpenzi wangu.

 

 

Mpaka Home: Ni kitu gani unapenda kukifanya ukiwa umepumzika nyumbani?

Mlela: Asikwambie mtu, mwanangu ndo’ kila kitu. Napenda kukaa na mwanangu kwa sababu ninampenda sana kwa kweli.

Mpaka Home: Ratiba yako kwa siku imekaaje?

Mlela: Nikiamka asubuhi ninafanya mazoezi. Baada ya hapo ninaandaa chai, ninakunywa kisha ninamsaidia mpenzi wangu kazi za nyumbani, kama kufanya usafi wa kufua na kupika, ndiyo mambo mengine yanaendelea na kama nina kazi, ninatoka.

 

 

Mpaka Home: Ukiwa nyumbani unapenda kula chakula gani?

Mlela: Napenda sana vyakula vya baharini, kama samaki na ugali au wali.

Mpaka Home: Je, huyo mpenzi wako anaitwa nani na unaonaje ukiwatambulisha mashabiki wako kwa kupiga naye picha?

 

 

Mlela: Siwezi kuweka jina lake wazi kwa sasa wala kumwanika kwa sababu muda muafaka haujafika, siku ikifika nitamtambulisha tu.

Mpaka Home: Mbali na mambo uliyoyataja hapo juu ambayo huwa unayafanya unapokuwa nyumbani, je, hakuna vingine unavyofanya vya tofauti?

Mlela: Napenda sana kuangalia runinga, kucheza gemu na kutunga stori za muvi zangu.

Mpaka Home: Kwa sasa soko la filamu limeshuka, je, unawezaje kuendesha maisha ya hapa nyumbani?

 

Mlela: Ni kweli, soko kwa sasa ni gumu sana, lakini ninaishi vizuri kutokana na kazi za tamthiliya ninazozifanya nchini Kenya. Moja ya tamthiliya hizo ni Nyota ambayo inaendelea kuruka kwenye Televisheni ya Azam na kwa kweli inapendwa sana.

Mpaka Home: Nashukuru kwa ushirikiano.

Mlela: Asante, karibu sana hapa ndiyo home.

 

MAKALA: GLADNESS MALLYA | RISASI JUMAMOSI| MPAKA HOME| DAR

Leave A Reply