The House of Favourite Newspapers

Haya Utayasikia Kwenye Documentary ya Chris Brown

0
Chris Brown

Inawezekana ulisubiri sana! Dogo anayefanya poa kwenye muziki kwa miaka kadhaa sasa, Chris Brown anajiandaa kutoa documentary yake ambayo itaelezea mambo mengi yakiwemo mahusiano yake na mtoto mkali ambaye pia ni mwanamuziki, Rihanna.

Watu wengi wamekuwa wakiisubiri documentary hiyo kwa kipindi kirefu kwani wanaamini kwamba itaelezea mambo mengi kuhusu staa huyo na ugomvi mkubwa na aliyekuwa mpenzi wake, Rihanna hali iliyompelekea kupelekwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka.

Ikumbukwe kwamba mara baada ya kuachana na mrembo huyo, akajikuta akianguka kwenye penzi la mwanadada Karrueche ila baadaye kukatoka taarifa kwamba alikuwa na mtoto kutoka kwa mwanamke mwingine.

Mambo yote hayo utayasikia kwenye documentary hiyo ambayo pia itahusisha shoo zake nyingi alizowahi kufanya. Wasanii wengi wamezungumza humo, kila kitu ulichokuwa na hamu ya kukisikia, utakisia.

Documentary hiyo inatarajiwa kuzinduliwa tarehe 8 mwezi ujao ambapo itauzwa sehemu mbalimbali ikiwemo katika Mtandao wa iTune ambao tayari nao wamehitaji kopi zao kwa ajili ya kufanya biashara.

 

Na: Nyemo Chilongani

Leave A Reply