The House of Favourite Newspapers

Wateja wa Vodacom Waletewa Bando la RED

0
Mkuu wa masoko na mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC, Nandi Mwiyombella (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wahabari (hawapopichani) wakati wauzinduzi wa huduma mpyaya RED inayojumuishwa vifurushi na huduma za kipekee nyingi, Vifurushi hivyo vina dakika nyingi, MB za intaneti nyingi, SMS nyingi na dakika za kupiga simu nje ya nchi pindi mteja akijiunga, Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar esSalaam,Wanaoshuhudia kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano w akampuni hiyo, Jacqueline Materuna Meneja wa maendeleo ya Uzalishaji wa masoko, Frank Madembwe.

Wateja wa Vodacom Tanzania kuanzia sasa watakuwa na furaha zaidi kwa keletewa huduma mpya ya RED. Huduma hii ni mpango unaojumuishwa vifurushi na  kulipa kadri utumiavyo. Vifurushi hivi vina dakika nyingi, MB za intaneti nyingi, SMS nyingi na pia dakika za kupiga simu nje ya nchi. Wakati mteja akinunua kifurushi cha RED, anaweza kuchagua huduma ya kifurushi cha kujirudia (kujinunua tena) kila kinapoisha muda wake au kununua mara moja tu.

Mteja yeyote yole wa Vodacom akinunua bando ya RED, atapata nafasi na kipaumbele ya kuhudumiwa bila kukaa kwenye foleni wakati akitembelea duka lolote la kampuni hiyo, ambayo yatakuwa na  madawati maalum ya RED yatakayokuwa yametengwa kwa ajili yao.

 

Kutoka kushoto Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusianowa Vodacom Tanzania, Jacqueline Materu, Mkuu wa masoko na mawasiliano wa kampuni hiyo, Nandi Mwiyombella na Meneja wamaendeleo ya Uzalishaji wa masoko, Frank Madembwe, wakionyesha ujumbe wa jinsi ya kujiunga na huduma mpya ya RED

 

Akiongea na waandishi wa habari jana wakati wa kuitambulisha huduma hiyo, Mkuu wa kitengo cha Masoko na Masiliano wa kampuni hiyo Nandi Mwiyombella alisema tumeamua kuileta huduma hii yakipekee sokoni kwa ajili ya wateja wetu huu ni mpango unaojumuishwa vifurushi na  kulipa kadri utumiavyo. Vifurushi hivi vina dakika nyingi, MB za intaneti nyingi, SMS nyingi na pia dakika za kupiga simu nje ya nchi. Wakati mteja ananunua anaweza kifurushi cha RED, anaweza kuchagua huduma ya kifurushi cha kujirudia (kujinunua tena) kila kinapoisha muda wake au kununua mara moja tu.

 

“Bando hii ya RED itapatikana kwa kununua kupitia USSD na itadumu kwa muda wa siku 30 kuanzia siku ambayo mteja ameinunua vile vile itakuwa na kipengele cha kujirudia ili kuongeza ufanisi na tunaelewa umuhumi wa kupata taarifa mbali mbali kwa wateja wetu. Wateja wa RED watapata taarifa bure baada ya kumaliza kuongea na simu kuashiria mwisho wa mazungumzo, taarifa ya simu ambazo haujapokea pamoja na matumizi ya data”alisema Mwiyombella.

 

Ili mteja ajiunge na kunufaika na kifurushi hichi anatakiwa kupiga *149*01# na Chagua RED na ataona vifurushi vyote vya RED

 

Ukishajiunga na RED utaweza kufurahia yafuatayo:-

 

Pamoja na mteja kupata dakika za maongezi za mitandao yote, vifurushi vya intaneti, SMS na dakika za kimataifa, pia atapata;

  • Huduma ya SOKONI App BURE
  • Taarifa fupi ya M-Pesa BURE pale atakapoihitaji
  • Huduma ya kipekee pindi atakapowasiliana na huduma kwa wateja.
  • Huduma ya kipekee, pindi atembeleapo maduka yetu ya Vodacom

 

Huduma ya kipekee, kitengo cha msaada Zaidi cha Vodacom

Leave A Reply