Heri ya Kuzaliwa Ghalib Said Mohamed-GSM, Mdhamini wa Klabu ya Yanga
LEO NOVEMBA 19, 2023 ni siku muhimu kwa Mfanyabiashara, Ghalib Said Mohamed (GSM) ambaye anasherehekea siku yake ya kuzaliwa na kipenzi cha mashabiki wa Yanga.
GSM ambaye ndiye mdhamini wa Jezi za Yanga ni moja ya watu walioleta chachu kubwa tangu aingie kwenye mpira.
Ameirudisha kwenye heshima Yanga na kuifanya kuwa moja ya timu vigogo barani Afrika.
Tunatambua mchango wako ni mkubwa kwa timu ya Yanga na Taifa, hivyo tunakuombea miaka mingi zaidi, Mwenyezi Mungu azidi kukulinda kaka na uendelee kutoa mchango wako mkubwa ndani ya Yanga na mpira wetu kwa Ujumla.
Heri ya Kuzaliwa Ghalib Said Mohamed (GSM)!