Exclusive: Kibibi Wa Huba Nimekulia Maisha Ya Uchokoraa, Mimi Ni Mzuri, Sijawahi Kumuona Idris Sultan – Video
Muigizaji mahiri wa tamthiliya ya Huba, Getrude Mwita @official_getrudemwita amefunguka kuwa, hawezi kuacha kumtukuza Mungu, kwasababu maisha aliyopitia mpaka alipo hivi sasa ni Mungu tu na kuwashukuru wazazi waliomchukua na kumlea.
” Kitu ambacho mpaka leo kinaniumiza sana kwenye maisha yangu ni maisha ya uchokoraa niliyoishi ya kuomba barabarani na kulala tu popote lakini Mungu, amenivusha kote na kunifanya hivi leo” alisema Kibibi.