The House of Favourite Newspapers

Higuain Kukiwasha Chelsea

Mshambuliaji Gonzalo Higuain

DIRISHA la usajili mdogo wa Januari linaendelea na taarifa ni kuwa Klabu ya Chelsea hadi kufikia jana mchana, ilikuwa katika hatua za mwisho kukamilisha mchakato wa kumsajili mshambuliaji Gonzalo Higuain kutoka AC Milan.

 

Dili la mchezaji huyo ambaye anaichezea timu hiyo kwa mkopo akitokea Juventus pia ni la mkopo ambapo likikamilika ataichezea Chelsea hadi mwishoni mwa msimu huu.

 

Higuain inadaiwa kuwa ameonyesha kuwa na nia ya wazi ya kuondoka Milan kwa ajili ya kupata ushindani mpya.

Iliele- zwa kuwa Chelsea ilikubali kumjumuisha mshambuliaji wao mwingine, Michy Batshuayi katika dili hilo ili wapishane. Dili hilo linaelekea kukamilika kwa kuwa Chelsea pia ilikuwa na mpango wa kumuuza Alvaro Morata kwenda Atletico Madrid.

 

Kocha wa Chelsea, Maurizio Sarri amekuwa akimhitaji Higuain kwa kuwa wawili hao waliwahi kufanya kazi pamoja wakiwa Napoli msimu wa 2015-16, ambapo Higuain alifunga mabao 36 katika mechi 35 za Serie A

Comments are closed.