Hii ndiyo Idadi ya wanaume wa Tanasha

DAR ES SALAAM: Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anafahamika kwa kucheza na mioyo ya watoto wa kike kisha kuwaacha solemba.  Kwa upande wake, mchumba wa Diamond au Mondi wa sasa, Tanasha Donna Oketch amejibu kuwa haogopi kutendwa kwani hata yeye huko nyuma aliwahi kuwa na wanaume wapatao watatu kabla ya kuwa na Mondi.

Tanasha alianika idadi hiyo ya wanaume wake ‘maeksi’ alipokuwa akijibu maswali ya mashabiki wake kupitia mitandao ya kijamii ambapo alisema hawezi kumhukumu Mondi kwa kuangalia historia yake. Alisema kuwa hana shida na Mondi kwani jamaa huyo anatimiza wajibu wake wa kumhudumia vyema na hata yeye alikuwa na wapenzi kabla ya kuwa na Mondi.

“Kila mtu ana historia yake na wapenzi wake waliopita. Hata mimi kabla ya kumjua (Mondi) nilikuwa na wapenzi. Ndiyo, nilishakuwa nao watatu kabla ya kuwa naye. Kwa hiyo siwezi kumhukumu kwa  kuangalia historia yake na mambo yake ya nyuma. Mimi ninaangali mtu alivyo sasa hivi. Kama ananijali vizuri, wala hakuna shida,” alisema Tanasha.

Mtangazaji huyo wa Kituo cha Redio cha NRG cha jijini Mombasa, Kenya alisema angependa kuzaa watoto wengi na Mondi. Tanasha anayetarajiwa kujifungua mwezi huu alisema baada ya kumzalia mtoto wa kwanza, atamzalia Mondi mtoto mwingine baada ya miaka kati ya mitano na saba


Loading...

Toa comment