The House of Favourite Newspapers

Hivi Ndivyo Jokate Alivyoonja Chungu, Tamu ya Maisha!

Mrembo Jokate Mwegelo,

WIKI hii ilikuwa moto kwelikweli Bongo, matukio mengi ya kitaifa na ya kiburudani yalitrend lakini miongoni mwayo ni lile la msanii wa wa filamu Bongo ambaye ni Miss Tanzania Bongo 2006, Wema Sepetu kuuanika ‘msambwanda’ wake akiwa anaogelea kwenye swimming pool.

Lingine ni lile la viongozi wa Chadema akiwemo mwenyekiti wake, Freeman Mbowe kulala katika Gereza la Segerea. (Zaidi soma ukurasa wa 2).

Ukiachana na hayo, tukio lingine kubwa ambalo lilitrend ni la kutumbuliwa kwa mrembo Jokate Mwegelo, katika Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM).

ILIKUWAJE?

Kutumbuliwa kwa Jokate, ni kitu ambacho wengi walionekana hawakuwa wanakitarajia, lakini mwishoni mwa wiki iliyopita hilo lilitokea baada ya kutangazwa kuwa mrembo huyo ameenguliwa katika uteuzi wa nafasi ya Kaimu Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa umoja huo, aliyokuwa akiishikilia toka Aprili, mwaka jana.

Kuhusu kutenguliwa kwake, Kaimu Katibu Mkuu Taifa wa Umoja wa UVCCM, Shaka Hamdu alikiri juu ya hilo, kwamba Jokate alitenguliwa Machi 25, mwaka huu kupitia vikao vya kamati vilivyokutana kwa mujibu wa kanuni na taratibu za UVCCM.

“Ifahamike Jokate aliteuliwa kukaimu kwa utaratibu wa UVCCM na ameondolewa kwa utaratibu pia, ni kama alikuwa kwenye majaribio na utaratibu wa kuijaza nafasi hiyo utafanyika hapo baadaye kupitia vikao vya umoja huo,” alisema Shaka.

Miss Tanzania Bongo 2006, Wema Sepetu

 

Shaka aliongeza kwamba uteuzi wa Jokate kuwa Kaimu Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi, ulionekana kutaka kuivuruga jumuiya hiyo baada ya kuibuka mjadala kwa viongozi na wanachama wakidai uteuzi huo haukufuata kanuni na taratibu za umoja huo.

NI BAADA YA BETHIDEI YAKE

Kutumbuliwa kwa Jokate, ilikuwa ni siku chache baada ya kusherehekea siku yake yake ya kuzaliwa huku akipokea zawadi mbalimbali za maua na keki.

Hazikuwa zimezidi siku tatu, ambapo baada ya uamuziki huo mijadala mbalimbali iliibuka pia kwenye mitandao ya kijamii na watu wakiwa na maoni tofautitofauti katika suala hilo.

WASHANGAZWA KUTENGULIWA KWAKE

Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii walionesha kushangazwa na suala la Jokate kutenguliwa kwani alikuwa anakaimu tu nafasi hiyo.

Msikie huyu Edward Clement Kyungu; “Kimsingi mtu anayekaimu huwa hatenguliwi zaidi kinachofanyika ni kumteua mtu mwingine ambaye ndiye atakuwa mwenye kushika hiyo nafasi, yaani ni kitendo cha kuteua tu mtu mwingine, kitendo cha kutengua kukaimu kwake wakati hajateuliwa mwingine wa kushika nafasi hiyo ni tatizo.”

Mijadala ilikuwa ni mingi na wengine walimtia zaidi moyo Jokate kuzidi kupambana kisiasa ili siku moja afike mbali.

JOKATE ATAFUTWA

Ijumaa lilimtafuta Jokate lakini simu yake iliita bila kupokelewa. Hata hivyo jitihada zilifanyika za kumtumia meseji kwa kirefu juu ya kutoa ufafanuzi wa sakata hilo lakini napo ilionesha kumfikia pasipo majibu.

MWENYEKITI WAKE ATAFUTWA

Ijumaa pia lilimtafuta Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM, Kheri James ambapo simu yake iliita tu bila kupokelewa.

Kwa upande wa msaidizi wake Antar Sangali, apopatikana baada ya kutafutwa alisema kwamba; “CCM ni taasisi, ina taratibu zake za watu wa kuzungumza. Sina mamlaka yoyote yale ya kueleza juu ya jambo hili.”

Gazeti la Ijumaa, lilimtafuta pia Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Shakha Hamdu, naye simu yake iliita tu na haikuweza kupokelewa.

MAKALA: BONIPHACE NGUMIJE

Comments are closed.