The House of Favourite Newspapers

Hotuba ya Rais Samia Ikulu ya Nairobi Kenya – Video

0

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo Mei 05, ameanza ziara ya siku mbili nchini Kenya ambapo mbali na kufanya shughuli mbalimbali akiwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, lakini pia atalihutubia Bunge la Kenya.

 

HOTUBA YA RAIS SAMIA IKULU YA NAIROBI, KENYA

“Nashukuru sana Rais Kenyatta kwa makaribisho mazuri, tumeongea mengi ila kubwa ni uhusiano, nimemwambia Kenyatta kuwa Kenya inashika nafasi ya 5 Duniani kwa uwekezaji Tanzania, imewekeza miradi 513 yenye thamani ya USD Bil 1.7 ambayo imetoa ajira 51,000 za Watanzania.

 

Tumejadili mambo mengi kama alivyosema Rais Kenyatta lakini kubwa ninalotaka kulisisitiza ni Uhusiano baina yetu. Nchi zetu sio tu majirani lakini ni Ndugu. Kenya imefanya uwekezaji Tanzania na kutoa ajira kwa wengi. Nimeweka ahadi Tanzania tutawekeza zaidi Kenya.

 

“Mwaka huu Desemba 12, Tanzania tunatimiza miaka 60 ya Uhuru wetu na nimetoa mwaliko rasmi kwa Rais Kenyatta awe Mgeni rasmi katika Maadhimisho yale ya miaka 60 ya Uhuru wetu.

 

“Naahidi Tanzania sasa tutakuja kwa nguvu yote Kenya kuja kuwekeza ili kukuza ujazo wa kibiashara, tuna fursa kubwa katika Nchi zetu sasa tunakwenda kutumia fursa hizi kukuza biashara kati ya Tanzania na Kenya na katika Mataifa mengine.

 

“Tumekubaliana kuendelea kushughulikia changamoto hususani vikwazo visivyo vya kodi vinavyojitokeza kwenye mipaka yetu tumekubaliana vikaondoke na kwa pamoja tumeitaka Tume yetu ya Makubaliano iwe inakaa na kutoa suluhu ya vikwazo hivyo.

 

Tumekubaliana kuwa Mawaziri wetu wa Afya watakaa na kuangalia jinsi ya kurahisisha mfumo wa kuingia na kuchekiwa maambukizi ya #CoronaVirus. Watu wetu wapate huduma ya kupimwa haraka ili huduma za biashara ziendelee.

Leave A Reply