The House of Favourite Newspapers

HOYCE TEMU ALIACHA KAZI BENKI ILI AISAIDIE JAMII

Image result for Hoyce Temu

Hoyce Temu MWAKA 1999 ni miongoni mwa miaka ambayo haitasahaulika kwenye kinyang’anyiro cha Miss Tanzania. Kwa waliobahatika kukishuhudia watakumbuka namna Miss Tanzania mteule, mzaliwa wa Arusha, Hoyce Temu alivyokuwa gumzo.  Gumzo lilitokana na mambo mengi, kwanza uzuri wa sura, umbo na hata alivyokuwa ‘smart’ kujibu maswali kutoka kwa majaji.

Lakini pia kilichonogesha zaidi ushindi wake ulikuwa ni Wimbo wa Miss Tanzania, uliotungwa na mwanamuziki Emmanuel Nkumila. Huu ni wimbo uliopendwa sana na baadhi ya mashairi ya mwanzo ya wimbo huo yalikuwa hivi; “Kila mahali jijini Dar es Salaam, hakuna mrembo kama weeeeweee… Mwanzo kuwa Twiga wa Maringo, nakuonaaeee, nashindwa kusema, maneno, oh! Mii…”

Baada ya kuvaa kofia ya Miss Tanzania, Hoyce Temu amekuwa na mchango mkubwa kwa jamii na amefanya mambo mengi ya kusaidia watu yaliyompa heshima, ungana hapa chini kujifunza baadhi ya vitu kutoka kwake kwenye safari ya kutimiza ndoto zake.Image result for Hoyce Temu

UNAJUA KUHUSU UREMBO KWA MALENGO?

Baada ya shindano la Miss Tanzania mwaka huu kwenye gazeti dada na hili, Uwazi nilieleza juu ya kitu kinachoitwa urembo kwa malengo. Nitarudia kwa kifupi.

Ipo hivi; Mwaka 1972, mwanamitindo Julia Morley ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa shirika linaloratibu mashindano ya Miss World alianzisha kitu kinaitwa ‘Beauty With Purpose’, yaani ‘Urembo kwa Malengo’ kwenye mashindano ya mamiss. Kwa miaka nenda rudi, Urembo kwa Malengo umekuwa ni moyo wa mashindano ya mamiss sehemu tofautitofauti duniani.

Ndiyo maana hata hapa kwetu katika kila mchakato wa mamiss utaona wanajihusisha kwenye shughuli mbalimbali za kijamii, na wengine huishi na nadharia hii ya urembo kwa malengo baada ya kutoka kwenye mchuano wa mamiss. Huutumia urembo wao kuinufaisha jamii.Image result for Hoyce Temu

Kwa upande wa Hoyce ameishi na kitu hiki miaka nenda rudi. Amewahi kuzungumza kwamba kwake zawadi ya gari, aliyoipata haikuwa tamati ya ndoto zake za kuwa Miss Tanzania. Tamati ilikuwa ni katika mambo ambayo anayafanya kwa sasa ya kuisaidia taifa.

JIULIZE UTAIFANYIA NINI TANZANIA, SIYO TANZANIA ITAKUFANYIA NINI!

Huu ni msemo mwingine ambao mwanadada huyu anapenda kuutumia. Kwamba kwa mtu yeyote unapokuwa katika safari ya kutimiza ndoto zako, jambo la kwanza ni kujiuliza unataka nini na mafanikio utakayoyapata yatakuwa na manufaa gani kwa watu wengine.

Kwa upande wake amewahi kuacha kazi benki ili tu afanye kazi za jamii. Yote hiyo ni kwa sababu alikuwa bado anaona hajaitendea haki Tanzania.Image result for Hoyce Temu

KUHUSU KAZI ZAKE ZA KIJAMII

Hoyce anaendesha kipindi kiitwacho Mimi na Tanzania ambacho kimekuwa msaada mkubwa kwa wagonjwa mbalimbali mijini na vijijini ambao wanakuwa hawana pesa za matibabu. Hoyce amekuwa akiwasaidia wagonjwa hao kupata pesa kwa kuchangisha kutoka kwa Watanzania wanaomuamini na kumuunga mkono na amekuwa akipeleka wagonjwa mpaka nje ya nchi.

Mbali na hilo Hoyce pia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa, hufanya kazi ya kuwasiliana na mashirika ya umoja wa mataifa na kuwashauri viongozi wa umoja wa mataifa na serikali ya Tanzania.Kipindi cha MiminaTanzania hakibagui, hakichaugui. Waliopo Mkoani Morogoro na wenye uhitaji wamefikiwa. #wenzetu #jamii #nchiyangu

HATA WEWE UNAWEZA KUFANYA MAKUBWA!

Hayo ni mambo machache tu kutoka kwa Mwanamke wa Chuma wa wiki hii Hoyce Temu. Ukweli ni kwamba yapo mengi sana ya kuzungumzia kumhusu mama huyu.

Amewahi kupata tuzo mbalimbali akiwa mwanamke shujaa na amefanya kazi nyingi kwa ajili ya jamii. Hata hivyo jambo lingine la kujifunza kutoka kwake ni kwamba amewahi kupitia maisha ya kawaida kabisa. Amewahi kuishi maisha ya kimasikini na sasa anaishi maisha ya ndoa.Kwa hiyo inawezekana kwa kila mmoja wetu. Kwa mwanadada unayesoma hapa unayo nafasi ya kufanya makubwa, kujenga imani yako na kuisaidia jamii kama Hoyce. Inuka na chukua hatua!

Comments are closed.